Yoshua 1:15 - Swahili Revised Union Version15 hadi BWANA atakapowapa ndugu zenu raha, kama alivyowapa ninyi, na wao pia wamepata kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu; ndipo mtakapoirudia nchi ya milki yenu na kuimiliki, ambayo Musa mtumishi wa BWANA aliwapeni ng'ambo ya Yordani upande wa maawio ya jua. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema15 Mtawasaidia mpaka Mwenyezi-Mungu atakapowapa ndugu zenu pia mahali pa kupumzikia, kama alivyowapa nyinyi, nao pia wamiliki nchi ambayo wanapewa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Kisha mtarudi katika nchi ambayo ni mali yenu na kuimiliki, nchi ambayo mlipewa na Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, mashariki ya mto Yordani.” Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND15 Mtawasaidia mpaka Mwenyezi-Mungu atakapowapa ndugu zenu pia mahali pa kupumzikia, kama alivyowapa nyinyi, nao pia wamiliki nchi ambayo wanapewa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Kisha mtarudi katika nchi ambayo ni mali yenu na kuimiliki, nchi ambayo mlipewa na Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, mashariki ya mto Yordani.” Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza15 Mtawasaidia mpaka Mwenyezi-Mungu atakapowapa ndugu zenu pia mahali pa kupumzikia, kama alivyowapa nyinyi, nao pia wamiliki nchi ambayo wanapewa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Kisha mtarudi katika nchi ambayo ni mali yenu na kuimiliki, nchi ambayo mlipewa na Mose, mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, mashariki ya mto Yordani.” Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu15 hadi Mwenyezi Mungu awape nao utulivu, kama alivyowatendea ninyi, hadi wao pia watakapokuwa wamemiliki nchi ile Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anayowapa. Baada ya hilo, mwaweza kurudi na kuimiliki nchi yenu wenyewe, ambayo Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu aliwapa mashariki mwa Yordani kuelekea linakochomoza jua.” Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu15 bwana awape nao raha, kama alivyokwisha kufanya kwa ajili yenu hadi wao pia watakapokuwa wamemiliki nchi ile bwana Mwenyezi Mungu wenu anayowapa. Baada ya hilo, mwaweza kurudi na kukalia nchi yenu wenyewe, ambayo Musa mtumishi wa bwana aliwapa mashariki mwa Yordani kuelekea linakochomoza jua.” Tazama suraBIBLIA KISWAHILI15 hadi BWANA atakapowapa ndugu zenu raha, kama alivyowapa ninyi, na wao pia wapate kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu; ndipo mtakapoirudia nchi ya milki yenu na kuimiliki, ambayo Musa mtumishi wa BWANA aliwapeni ng'ambo ya Yordani upande wa mawio ya jua. Tazama sura |