Abrahamu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu.
Yona 3:3 - Swahili Revised Union Version Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake ni mwendo wa siku tatu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Yona akaondoka, akaenda Ninewi kama Mwenyezi-Mungu alivyomwagiza. Mji wa Ninewi ulikuwa mkubwa sana. Upana wake ulikuwa mwendo wa siku tatu. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Yona akaondoka, akaenda Ninewi kama Mwenyezi-Mungu alivyomwagiza. Mji wa Ninewi ulikuwa mkubwa sana. Upana wake ulikuwa mwendo wa siku tatu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Yona akaondoka, akaenda Ninewi kama Mwenyezi-Mungu alivyomwagiza. Mji wa Ninewi ulikuwa mkubwa sana. Upana wake ulikuwa mwendo wa siku tatu. Neno: Bibilia Takatifu Yona akalitii neno la Mwenyezi Mungu naye akaenda Ninawi. Basi Ninawi ulikuwa mji maarufu sana, ilichukua siku tatu kuuzunguka. Neno: Maandiko Matakatifu Yona akalitii neno la bwana naye akaenda Ninawi. Basi Ninawi ulikuwa mji maarufu sana, ilichukua siku tatu kuuzunguka. BIBLIA KISWAHILI Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake ni mwendo wa siku tatu. |
Abrahamu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu.
Raheli akasema, Kwa mashindano makuu nimeshindana na dada yangu, nikashinda. Akamwita jina lake Naftali.
Haki yako ni kama milima ya Mungu, Hukumu zako ni vilindi vikuu, Ee BWANA, unawalinda wanadamu na wanyama.
Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu.
na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya elfu mia moja na ishirini, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?
Luka peke yake yupo hapa pamoja nami. Umtwae Marko, umlete pamoja nawe, maana anifaa kwa utumishi.