ili kuzithibitisha siku hizo za Purimu kwa majira yake, kama Mordekai Myahudi na malkia Esta walivyoamuru, na kama walivyojiagizia juu yao wenyewe, na juu ya wazawa wao, kwa kufunga na kulia.
Yona 3:2 - Swahili Revised Union Version Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Nenda Ninewi, ule mji mkuu, ukawatangazie watu ujumbe niliokupa.” Biblia Habari Njema - BHND “Nenda Ninewi, ule mji mkuu, ukawatangazie watu ujumbe niliokupa.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Nenda Ninewi, ule mji mkuu, ukawatangazie watu ujumbe niliokupa.” Neno: Bibilia Takatifu “Ondoka uende katika mji mkubwa wa Ninawi, ukautangazie ujumbe ninaokupa.” Neno: Maandiko Matakatifu “Ondoka uende katika mji mkubwa wa Ninawi, ukautangazie ujumbe ninaokupa.” BIBLIA KISWAHILI Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru. |
ili kuzithibitisha siku hizo za Purimu kwa majira yake, kama Mordekai Myahudi na malkia Esta walivyoamuru, na kama walivyojiagizia juu yao wenyewe, na juu ya wazawa wao, kwa kufunga na kulia.
Musa akamwambia Haruni hayo maneno yote ya BWANA ambayo alimtuma aende nayo, na ishara hizo zote alizomwagiza.
Haya basi, wewe jifunge viuno, ukaondoke ukawaambie maneno yote niliyokuamuru; usifadhaike kwa ajili yao, nisije nikakufadhaisha wewe mbele yao.
Lakini BWANA akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru.
Nawe utawaambia maneno yangu, iwe watasikia au hawataki kusikia; maana hao wanaasi sana.
Mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi wa nyumba ya Israeli; basi, sikia neno hili litokalo katika kinywa changu, ukawape maonyo haya yatokayo kwangu.
Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu.
Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake ni mwendo wa siku tatu.
Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.