Yohana 9:6 - Swahili Revised Union Version Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope machoni, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baada ya kusema hayo, akatema mate chini, akafanyiza tope, akampaka yule kipofu machoni, Biblia Habari Njema - BHND Baada ya kusema hayo, akatema mate chini, akafanyiza tope, akampaka yule kipofu machoni, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baada ya kusema hayo, akatema mate chini, akafanyiza tope, akampaka yule kipofu machoni, Neno: Bibilia Takatifu Baada ya kusema haya, akatema mate ardhini, akatengeneza tope kwa mate na kumpaka yule kipofu machoni. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya kusema haya, akatema mate ardhini, akatengeneza tope kwa mate na kumpaka yule mtu kipofu machoni. BIBLIA KISWAHILI Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope machoni, |
Akamtenga na mkutano faraghani, akatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi,
Akamshika mkono yule kipofu, akamchukua nje ya kijiji, akamtemea mate katika macho, akamwekea mikono yake, akamwuliza, Waona kitu?
Yeye akajibu, Mtu yule aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka macho akaniambia, Nenda Siloamu ukanawe; basi nikaenda na kunawa, nikapata kuona.
Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona.