Kama vile wewe usipojua njia ya upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni mwake mja mzito; kadhalika huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote.
Yohana 9:10 - Swahili Revised Union Version Basi wakamwambia, Macho yako yalifumbuliwaje? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, wakamwuliza, “Sasa, macho yako yalipataje kufumbuliwa?” Biblia Habari Njema - BHND Basi, wakamwuliza, “Sasa, macho yako yalipataje kufumbuliwa?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, wakamwuliza, “Sasa, macho yako yalipataje kufumbuliwa?” Neno: Bibilia Takatifu Wakamuuliza, “Basi macho yako yalifumbuliwaje?” Neno: Maandiko Matakatifu Wakamuuliza, “Basi macho yako yalifumbuliwaje?” BIBLIA KISWAHILI Basi wakamwambia, Macho yako yalifumbuliwaje? |
Kama vile wewe usipojua njia ya upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni mwake mja mzito; kadhalika huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote.
Wakamwuliza Baruku, wakisema, Tuambie sasa; ulipataje kuyaandika maneno haya yote kinywani mwake?
Yeye akajibu, Mtu yule aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka macho akaniambia, Nenda Siloamu ukanawe; basi nikaenda na kunawa, nikapata kuona.
Basi Mafarisayo nao wakamwuliza tena jinsi gani alivyopata kuona. Akawaambia, Alinitia tope juu ya macho, nami nikanawa, na sasa naona.
lakini jinsi aonavyo sasa hatujui; wala hatujui ni nani aliyemfumbua macho. Mwulizeni yeye mwenyewe; yeye ni mtu mzima; atajisemea mwenyewe.
Wengine wakasema, Ndiye. Wengine wakasema, La, lakini amefanana naye. Yeye mwenyewe alisema, Mimi ndiye.