mkawaketishe watu wawili, watu walaghai, ili wamshitaki, na kumshuhudia, kunena, Umemtukana Mungu na mfalme. Kisha mchukueni nje, mkampige kwa mawe, ili afe.
Yohana 8:17 - Swahili Revised Union Version Tena katika torati yenu imeandikwa kwamba, Ushuhuda wa watu wawili ni kweli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Imeandikwa katika sheria yenu ya kwamba ushahidi wa watu wawili ni halali. Biblia Habari Njema - BHND Imeandikwa katika sheria yenu ya kwamba ushahidi wa watu wawili ni halali. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Imeandikwa katika sheria yenu ya kwamba ushahidi wa watu wawili ni halali. Neno: Bibilia Takatifu Imeandikwa katika Torati yenu kwamba ushahidi wa watu wawili ni thabiti. Neno: Maandiko Matakatifu Imeandikwa katika Torati yenu kwamba ushahidi wa watu wawili ni thabiti. BIBLIA KISWAHILI Tena katika torati yenu imeandikwa kwamba, Ushuhuda wa watu wawili ni kweli. |
mkawaketishe watu wawili, watu walaghai, ili wamshitaki, na kumshuhudia, kunena, Umemtukana Mungu na mfalme. Kisha mchukueni nje, mkampige kwa mawe, ili afe.
Mtu yeyote atakayemwua mtu, huyo mwuaji atauawa kwa vinywa vya mashahidi; lakini shahidi mmoja hatashuhudia juu ya mtu akauliwa.
La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.
Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu?
Hii ndiyo mara yangu ya tatu kuja kwenu. Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa.
Huyo atakayeuawa na auawe kwa midomo ya mashahidi wawili, au mashahidi watatu; asiuawe kwa mdomo wa shahidi mmoja. Ebr 10:28
Shahidi mmoja asimwinukie mtu awaye yote kumshuhudia kwa uovu wowote, wala kwa dhambi yoyote, katika makosa akosayo yoyote; jambo na lithibitishwe kwa vinywa vya mashahidi wawili, au watatu.
Mtu aliyeidharau Sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.
Kisha wako watatu washuhudiao duniani], Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja. Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe.
Nami nitawaruhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na mia mbili na sitini, wakiwa wamevikwa magunia.