Yohana 7:13 - Swahili Revised Union Version Lakini hakuna mtu aliyemsema waziwazi, kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hata hivyo hakuna mtu aliyethubutu kusema habari zake hadharani kwa kuwaogopa viongozi wa Wayahudi. Biblia Habari Njema - BHND Hata hivyo hakuna mtu aliyethubutu kusema habari zake hadharani kwa kuwaogopa viongozi wa Wayahudi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hata hivyo hakuna mtu aliyethubutu kusema habari zake hadharani kwa kuwaogopa viongozi wa Wayahudi. Neno: Bibilia Takatifu Lakini hakuna mtu yeyote aliyemsema waziwazi kwa sababu ya kuwaogopa viongozi wa Wayahudi. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini hakuna mtu yeyote aliyemsema waziwazi kumhusu kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi. BIBLIA KISWAHILI Lakini hakuna mtu aliyemsema waziwazi, kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi. |
Hata baada ya hayo Yusufu wa Arimathaya, naye ni mwanafunzi wa Yesu, (lakini kwa siri, kwa hofu ya Wayahudi), alimwomba Pilato ruhusa ili auondoe mwili wake Yesu. Na Pilato akampa ruhusa. Basi akaenda, akauondoa mwili wake.
Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu.
Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, tunajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye.
Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Yudea, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitaka kumwua.
Wazazi wake waliyasema hayo kwa sababu waliwaogopa Wayahudi; kwa maana Wayahudi walikuwa wamekwisha kukubaliana kwamba mtu akimkiri kuwa ni Kristo, atatengwa na sinagogi.
Wakajibu, wakamwambia, Ama! Wewe ulizaliwa katika dhambi tupu, nawe unatufundisha sisi? Wakamtoa nje.
Ninapajua ukaapo, ndipo penye kiti cha enzi cha Shetani; nawe unalishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hata katika siku za Antipa shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.