Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yohana 5:46 - Swahili Revised Union Version

Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Kama kweli mngemwamini Mose, mngeniamini na mimi pia, maana Mose aliandika juu yangu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Kama kweli mngemwamini Mose, mngeniamini na mimi pia, maana Mose aliandika juu yangu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Kama kweli mngemwamini Mose, mngeniamini na mimi pia, maana Mose aliandika juu yangu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kama mngemwamini Musa, mngeniamini na mimi, kwa maana aliandika habari zangu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kama mngelimwamini Musa, mngeliniamini na mimi kwa maana aliandika habari zangu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yohana 5:46
21 Marejeleo ya Msalaba  

nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.


ikiwa Abrahamu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa?


na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.


Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa.


nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.


Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.


Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.


Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti.


Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini maneno yangu vipi?


Basi kwa kuwa nimeupata msaada utokao kwa Mungu nimesimama hata leo hivi nikiwashuhudia wadogo kwa wakubwa, wala sisemi neno ila yale ambayo manabii na Musa waliyasema, kwamba yatakuwa;


Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki.


Maana mimi kwa njia ya sheria niliifia sheria ili nimwishie Mungu.


Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati, ayafanye.


Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;


Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani.


BWANA, Mungu wako, atakupa nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye.