Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.
Yohana 4:41 - Swahili Revised Union Version Watu wengi zaidi wakaamini kwa sababu ya neno lake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wengi zaidi waliamini kwa sababu ya ujumbe wake. Biblia Habari Njema - BHND Watu wengi zaidi waliamini kwa sababu ya ujumbe wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wengi zaidi waliamini kwa sababu ya ujumbe wake. Neno: Bibilia Takatifu Kwa sababu ya neno lake, watu wengi wakaamini. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa sababu ya neno lake, watu wengi wakaamini. BIBLIA KISWAHILI Watu wengi zaidi wakaamini kwa sababu ya neno lake. |
Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.
Wakamwambia yule mwanamke, Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu; maana sisi tumesikia wenyewe, tena tunajua ya kuwa hakika huyu ndiye Mwokozi wa ulimwengu.
Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na kote katika Yudea, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Basi, wakisafirishwa na kanisa, wakapita kati ya nchi ya Foinike na Samaria, wakitangaza habari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana.
Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri Habari Njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.
Nao walipokwisha kushuhudia na kulihubiri neno la Bwana wakarudi Yerusalemu, wakaihubiri Injili katika vijiji vingi vya Wasamaria.
Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, maana vitu vyote ni tupu na kuwekwa wazi machoni pake yeye ambaye tunapaswa kuwajibika kwake.