Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Matendo 8:12 - Swahili Revised Union Version

12 Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri Habari Njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Lakini walipouamini ujumbe wa Filipo juu ya Habari Njema ya ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo, walibatizwa, wanawake na wanaume.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Lakini walipouamini ujumbe wa Filipo juu ya Habari Njema ya ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo, walibatizwa, wanawake na wanaume.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Lakini walipouamini ujumbe wa Filipo juu ya Habari Njema ya ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo, walibatizwa, wanawake na wanaume.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Lakini watu walipomwamini Filipo akihubiri Injili ya ufalme wa Mungu na jina la Isa Al-Masihi, wakabatizwa, wanaume na wanawake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Lakini watu walipomwamini Filipo alipohubiri habari njema za Ufalme wa Mwenyezi Mungu na jina la Isa Al-Masihi, wakabatizwa wanaume na wanawake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

12 Lakini walipomwamini Filipo, akizihubiri Habari Njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.

Tazama sura Nakili




Matendo 8:12
22 Marejeleo ya Msalaba  

Basi, nendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;


Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, na kuponya wagonjwa.


Akamwambia Waache wafu wawazike wafu wao; bali wewe nenda ukautangaze ufalme wa Mungu.


wale aliojidhihirisha kwao kuwa yu hai, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, akiwatokea muda wa siku arubaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu.


Lakini baadhi ya hao walikuwa watu wa Kipro na Kirene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wayahudi wa Kigiriki, wakihubiri Habari Njema za Bwana Yesu.


Na Krispo, mkuu wa sinagogi, akamwamini Bwana pamoja na nyumba yake yote. Wakorintho wengi waliposikia, waliamini, wakabatizwa.


Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.


Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.


Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapatao elfu tatu.


nikiwashuhudia Wayahudi na Wagiriki wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo.


Na sasa, tazameni, mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowahubiria ufalme wa Mungu, nikienda huku na huko, hamtaniona uso tena.


akihubiri habari za ufalme wa Mungu, na kuyafundisha mambo ya Bwana Yesu Kristo, kwa ujasiri mwingi, asikatazwe na mtu.


walioamini wakazidi kuongezeka kwa Bwana, wengi, wanaume na wanawake;


Lakini wale waliotawanyika wakaenda huku na huko wakilihubiri neno.


Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.


Lakini, katika Bwana si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke.


Hakuna Myahudi wala Mgiriki. Hakuna mtumwa wala huru. Hakuna mwanamume wala mwanamke. Maana ninyi nyote mmekuwa wamoja katika Kristo Yesu.


Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo