Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng'ombe, na watumwa, na wajakazi?
Yohana 4:19 - Swahili Revised Union Version Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii! Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huyo Mwanamke akamwambia, “Bwana, naona ya kuwa wewe u nabii. Biblia Habari Njema - BHND Huyo Mwanamke akamwambia, “Bwana, naona ya kuwa wewe u nabii. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huyo Mwanamke akamwambia, “Bwana, naona ya kuwa wewe u nabii. Neno: Bibilia Takatifu Yule mwanamke akasema, “Bwana, naona bila shaka wewe ni nabii. Neno: Maandiko Matakatifu Yule mwanamke akasema, “Bwana, naona bila shaka wewe ni nabii. BIBLIA KISWAHILI Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii! |
Akamwambia, Je! Moyo wangu haukuenda na wewe, hapo alipogeuka yule mtu katika gari ili akulaki? Je! Huu ndio wakati wa kupokea fedha, na kupokea mavazi, na mashamba ya mizeituni, na mizabibu, na kondoo, na ng'ombe, na watumwa, na wajakazi?
Mmojawapo wa watumishi wake akasema, La, bwana wangu, mfalme; lakini Elisha, yule nabii aliye katika Israeli, humwambia mfalme wa Israeli maneno uyanenayo katika chumba chako cha kulala.
Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote;
Hofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu; na, Mungu amewaangalia watu wake.
Basi, yule Farisayo aliyemwalika alipoona vile, alisema moyoni mwake, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angemtambua mwanamke huyu amgusaye, ni nani, naye ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi.
kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli.
Njoni, mtazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! Inawezekana kuwa huyu ndiye Kristo?
Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni.
Basi wengine katika mkutano walipoyasikia maneno hayo, walisema, Hakika huyu ndiye nabii yule.
Basi wakamwambia yule kipofu mara ya pili, Wewe wasemaje kuhusu habari zake kwa vile alivyokufumbua macho? Akasema, Ni nabii.
BWANA, Mungu wako, atakupa nabii miongoni mwa ndugu zako kama nilivyo mimi; msikilizeni yeye.