Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa mhuri na Baba, yaani, Mungu.
Yohana 3:33 - Swahili Revised Union Version Yeye aliyeukubali ushuhuda wake ametia mhuri ya kwamba Mungu ni kweli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini mtu yeyote anayekubali ujumbe wake anathibitisha kwamba Mungu ni kweli. Biblia Habari Njema - BHND Lakini mtu yeyote anayekubali ujumbe wake anathibitisha kwamba Mungu ni kweli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini mtu yeyote anayekubali ujumbe wake anathibitisha kwamba Mungu ni kweli. Neno: Bibilia Takatifu Lakini yeyote anayekubali huo ushuhuda anathibitisha kwamba, Mungu ni kweli. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini yeyote anayekubali huo ushuhuda anathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu ni kweli. BIBLIA KISWAHILI Yeye aliyeukubali ushuhuda wake ametia mhuri ya kwamba Mungu ni kweli. |
Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa mhuri na Baba, yaani, Mungu.
Ninayo mengi ya kusema na kuhukumu juu yenu; lakini yeye aliyenituma ni kweli, nami niliyoyasikia kwake, ndiyo ninenayo katika ulimwengu.
Basi nikiisha kuimaliza kazi hiyo, na kuwatilia mhuri tunda hilo, nitapitia kwenu, kwenda Spania.
Naye aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, mhuri wa ile haki ya imani aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa; apate kuwa baba yao wote waaminio, ijapokuwa hawakutahiriwa, ili na wao pia wahesabiwe haki;
Kwa maana ikiwa mimi si mtume kwa wengine, lakini ni mtume kwenu ninyi; kwa maana ninyi ndinyi mhuri wa utume wangu katika Bwana.
Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, Habari Njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa mhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu.
Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa mhuri hata siku ya ukombozi.
Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye mhuri huu, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila aliitaye jina la Bwana na auache uovu.
Katika neno hilo Mungu, akitaka kuwaonesha zaidi sana warithio ile ahadi, jinsi mashauri yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati;
Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, tunamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo ndani yetu.