Akatoka nje yule aliyekufa, akiwa amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.
Yohana 20:5 - Swahili Revised Union Version Akainama na kuchungulia, akaona vitambaa vya sanda vimelala; lakini hakuingia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alipoinama na kuchungulia ndani, aliona sanda, lakini hakuingia ndani. Biblia Habari Njema - BHND Alipoinama na kuchungulia ndani, aliona sanda, lakini hakuingia ndani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alipoinama na kuchungulia ndani, aliona sanda, lakini hakuingia ndani. Neno: Bibilia Takatifu Akainama na kuchungulia mle kaburini, akaona vile vitambaa vya kitani, lakini hakuingia. Neno: Maandiko Matakatifu Alipofika, akainama na kuchungulia mle kaburini, akaona vile vitambaa vya kitani mle ndani, lakini hakuingia. BIBLIA KISWAHILI Akainama na kuchungulia, akaona vitambaa vya sanda vimelala; lakini hakuingia. |
Akatoka nje yule aliyekufa, akiwa amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia, Mfungueni, mkamwache aende zake.
Basi wakautwaa mwili wake Yesu, wakaufunga sanda ya kitani pamoja na yale manukato, kama ilivyo desturi ya Wayahudi katika kuzika.
Lakini Mariamu alikuwa akisimama karibu na kaburi, nje yake, analia. Wakati alipokuwa akilia, aliinama na kuchungulia ndani ya kaburi.
Wakaenda mbio wote wawili; na yule mwanafunzi mwingine akaenda mbio upesi kuliko Petro, akawa wa kwanza kufika kaburini.