Kwa kuwa nawaambia, hayo yaliyoandikwa hayana budi kutimizwa kwangu; ya kuwa, Alihesabiwa pamoja na wahalifu. Kwa sababu yanipasayo yanao mwisho wake.
Yohana 17:4 - Swahili Revised Union Version Mimi nimekutukuza duniani, nikiwa nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mimi nimekutukuza hapa duniani; nimeikamilisha ile kazi uliyonipa niifanye. Biblia Habari Njema - BHND Mimi nimekutukuza hapa duniani; nimeikamilisha ile kazi uliyonipa niifanye. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mimi nimekutukuza hapa duniani; nimeikamilisha ile kazi uliyonipa niifanye. Neno: Bibilia Takatifu Nimekutukuza wewe duniani kwa kuitimiza ile kazi uliyonipa niifanye. Neno: Maandiko Matakatifu Nimekutukuza wewe duniani kwa kuitimiza ile kazi uliyonipa niifanye. BIBLIA KISWAHILI Mimi nimekutukuza duniani, nikiwa nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye. |
Kwa kuwa nawaambia, hayo yaliyoandikwa hayana budi kutimizwa kwangu; ya kuwa, Alihesabiwa pamoja na wahalifu. Kwa sababu yanipasayo yanao mwisho wake.
Baba, ulitukuze jina lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.
Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, twendeni zetu.
Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake.
Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.
Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.
Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenituma, nikaimalize kazi yake.
Lakini ushuhuda nilio nao mimi ni mkuu kuliko ule wa Yohana; kwa kuwa zile kazi alizonipa Baba ili nizimalize, kazi hizo zenyewe ninazozitenda, zanishuhudia ya kwamba Baba amenituma.
Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.
Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu.