Ikawa baada ya hayo, Absalomu akajiwekea tayari gari na farasi, na watu hamsini wa kupiga mbio mbele yake.
Yohana 12:15 - Swahili Revised Union Version Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwanapunda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Usiogope mji wa Siyoni! Tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwanapunda!” Biblia Habari Njema - BHND “Usiogope mji wa Siyoni! Tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwanapunda!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Usiogope mji wa Siyoni! Tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwanapunda!” Neno: Bibilia Takatifu “Usiogope, ewe Binti Sayuni; tazama, mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda!” Neno: Maandiko Matakatifu “Usiogope, Ewe binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda!” BIBLIA KISWAHILI Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwanapunda. |
Ikawa baada ya hayo, Absalomu akajiwekea tayari gari na farasi, na watu hamsini wa kupiga mbio mbele yake.
Mfalme akamwambia Siba, Ni za nini hizi? Siba akasema, Punda ni za jamaa ya mfalme wazipande; na mkate na matunda ni chakula cha hawa vijana; na divai ni kwamba wanywe hao wazimiao nyikani.
Naye mfalme akawaambia, Twaeni pamoja nanyi watumishi wa bwana wenu, mkampandishe Sulemani mwanangu juu ya nyumbu wangu mimi mkamteremshe mpaka Gihoni;
Usiogope, Yakobo uliye mdudu, nanyi watu wa Israeli; mimi nitakusaidia, asema BWANA, na mkombozi wako ni Mtakatifu wa Israeli.
Tazama, BWANA ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia, Mwambieni binti Sayuni, Tazama, wokovu wako unakuja; Tazama, thawabu yake iko pamoja naye, Na malipo yake yako mbele zake.
Na wewe, Ee mnara wa kundi, kilima cha binti Sayuni, utajiliwa; naam, mamlaka ya kwanza yatakuja, ufalme wa binti Yerusalemu.
Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwanapunda, mtoto wa punda.
Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, Mpole, naye amepanda punda, Na mwanapunda, mtoto wa punda.
Ila asifanye farasi wake kuwa wengi, wala asiwarudishe watu Misri, ili apate kufanya farasi kuwa wengi; kwa kuwa BWANA amewaambia, Tangu sasa msirudie tena njia ile.
Naye alikuwa na wana arubaini, na wajukuu thelathini, waliokuwa wakipanda wanapunda sabini; akawa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka minane.
Itangazeni habari, ninyi mpandao punda weupe, Ninyi mketio juu ya mazulia ya thamani, Na ninyi mnaopita njiani kwa miguu.