Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yohana 11:3 - Swahili Revised Union Version

Basi wale dada wakatuma ujumbe kwake wakisema, Bwana, yeye umpendaye ni mgonjwa.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Basi, hao dada wakatuma ujumbe huu kwa Yesu: “Bwana, rafiki yako ni mgonjwa!”

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Basi, hao dada wakatuma ujumbe huu kwa Yesu: “Bwana, rafiki yako ni mgonjwa!”

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Basi, hao dada wakatuma ujumbe huu kwa Yesu: “Bwana, rafiki yako ni mgonjwa!”

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Hivyo hawa dada wawili walituma ujumbe kwa Isa kumwambia, “Bwana, yule umpendaye ni mgonjwa.”

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Hivyo hawa dada wawili walituma ujumbe kwa Isa kumwambia, “Bwana Isa, yule umpendaye ni mgonjwa.”

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Basi wale dada wakatuma ujumbe kwake wakisema, Bwana, yeye umpendaye ni mgonjwa.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yohana 11:3
16 Marejeleo ya Msalaba  

Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.


Nao watakatifu waliopo duniani, ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.


Bwana alipomwona alimwonea huruma, akamwambia, Usilie.


Basi mtu mmoja alikuwa mgonjwa, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake.


Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu, Lazaro, amelala; lakini ninakwenda nipate kumwamsha.


Ndiye Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu kwa nywele zake, ambaye Lazaro nduguye alikuwa mgonjwa.


Basi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa.


Basi Wayahudi wakasema, Angalieni jinsi alivyompenda.


Naye Yesu alimpenda Martha na dada yake na Lazaro.


Ninyi mwaniita, Mwalimu, na, Bwana; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo.


Na palikuwapo mmoja wa wanafunzi wake, ameegama kifuani pa Yesu, ambaye Yesu alimpenda.


Erasto alibaki Korintho. Trofimo nilimwacha huku Mileto, mgonjwa.


Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.