Musa akamlilia BWANA, akisema, Niwatendee nini watu hawa? Bado kidogo nao watanipiga kwa mawe.
Yohana 10:31 - Swahili Revised Union Version Basi Wayahudi wakaokota mawe tena ili wampige. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Wayahudi wakachukua mawe ili wamtupie. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Wayahudi wakachukua mawe ili wamtupie. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Wayahudi wakachukua mawe ili wamtupie. Neno: Bibilia Takatifu Kwa mara nyingine Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo, Neno: Maandiko Matakatifu Kwa mara nyingine Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo, BIBLIA KISWAHILI Basi Wayahudi wakaokota mawe tena ili wampige. |
Musa akamlilia BWANA, akisema, Niwatendee nini watu hawa? Bado kidogo nao watanipiga kwa mawe.
Wale wakulima wakawakamata watumwa wake, huyu wakampiga, na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe.
hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria mwana wa Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu.
Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani?
Basi Wayahudi walimzunguka, wakamwambia, Hata lini utatuhangaisha nafsi zetu? Kama wewe ndiwe Kristo, utuambie waziwazi.
Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonesha, zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe?
Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi, juzi juzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena?
Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Basi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambia,
Ni yupi katika manabii ambaye baba zenu hawakumwudhi? Nao waliwaua wale waliotabiri habari za kuja kwake yule Mwenye Haki; ambaye ninyi sasa mmekuwa wasaliti wake, mkamwua;
Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika BWANA, Mungu wake.