Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule?
Yohana 10:19 - Swahili Revised Union Version Kukawa na utengano tena kati ya Wayahudi, kwa ajili ya maneno hayo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kukawa tena na mafarakano kati ya Wayahudi kwa sababu ya maneno haya. Biblia Habari Njema - BHND Kukawa tena na mafarakano kati ya Wayahudi kwa sababu ya maneno haya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kukawa tena na mafarakano kati ya Wayahudi kwa sababu ya maneno haya. Neno: Bibilia Takatifu Waliposikia maneno haya, Wayahudi wakagawanyika. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maneno haya Wayahudi waligawanyika. BIBLIA KISWAHILI Kukawa na utengano tena kati ya Wayahudi, kwa ajili ya maneno hayo. |
Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule?
Basi baadhi ya Mafarisayo wakasema, Mtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato. Wengine wakasema, Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo? Kukawa na utengano kati yao.
Lakini jamii ya watu wa mjini wakafarakana; hawa walikuwa upande wa Wayahudi, na hawa upande wa mitume.
Kwa maana kwanza mnapokutanika kanisani nasikia kuna migawanyiko kwenu; nami kwa kiasi fulani naamini;
kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?