Kabla jua, na nuru, na mwezi, Na nyota, havijatiwa giza; Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua;
Yoeli 3:15 - Swahili Revised Union Version Jua na mwezi vimetiwa giza, na nyota zimeacha kuangaza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Jua na mwezi vinatiwa giza, na nyota zimeacha kuangaza. Biblia Habari Njema - BHND Jua na mwezi vinatiwa giza, na nyota zimeacha kuangaza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Jua na mwezi vinatiwa giza, na nyota zimeacha kuangaza. Neno: Bibilia Takatifu Jua na mwezi vitatiwa giza, na nyota hazitatoa mwanga wake tena. Neno: Maandiko Matakatifu Jua na mwezi vitatiwa giza, na nyota hazitatoa mwanga wake tena. BIBLIA KISWAHILI Jua na mwezi vimetiwa giza, na nyota zimeacha kuangaza. |
Kabla jua, na nuru, na mwezi, Na nyota, havijatiwa giza; Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua;
Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.
Nami nitakapokuzimisha, nitazifunika mbingu, na kuzifanya nyota zake kuwa giza; nami nitalifunika jua kwa wingu, wala mwezi hautatoa nuru yake.
Nchi inatetemeka mbele yao; mbingu zinatetemeka; jua na mwezi hutiwa giza, na nyota huacha kuangaza;
Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya BWANA iliyo kuu na itishayo.
Lakini mara tu, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka kutoka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika;
Lakini siku zile, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hatautoa mwanga wake.
Malaika wa nne akapiga baragumu, theluthi ya jua ikapigwa, na theluthi ya mwezi, na theluthi ya nyota, ili kwamba ile theluthi itiwe giza, mchana usiangaze theluthi yake, na usiku vivyo hivyo.