Yoeli 2:22 - Swahili Revised Union Version Msiogope, enyi wanyama wa porini; maana malisho ya jangwani yanatoa miche, na huo mti unazaa matunda yake, mtini na mzabibu inatoa nguvu zake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Msiogope, enyi wanyama. malisho ya nyikani yamekuwa mazuri, miti inazaa matunda yake, mizabibu na mitini zinazaa kwa wingi. Biblia Habari Njema - BHND Msiogope, enyi wanyama. malisho ya nyikani yamekuwa mazuri, miti inazaa matunda yake, mizabibu na mitini zinazaa kwa wingi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Msiogope, enyi wanyama. malisho ya nyikani yamekuwa mazuri, miti inazaa matunda yake, mizabibu na mitini zinazaa kwa wingi. Neno: Bibilia Takatifu Msiogope, enyi wanyama pori, kwa kuwa mbuga za malisho yenu zinarudia ubichi. Miti nayo inazaa matunda, mtini na mzabibu inatoa utajiri wake. Neno: Maandiko Matakatifu Msiogope, enyi wanyama pori, kwa kuwa mbuga za malisho yenu zinarudia ubichi. Miti nayo inazaa matunda, mtini na mzabibu inatoa utajiri wake. BIBLIA KISWAHILI Msiogope, enyi wanyama wa porini; maana malisho ya jangwani yanatoa miche, na huo mti unazaa matunda yake, mtini na mzabibu inatoa nguvu zake. |
Haki yako ni kama milima ya Mungu, Hukumu zako ni vilindi vikuu, Ee BWANA, unawalinda wanadamu na wanyama.
Na malisho yamejawa na kondoo, Na mabonde yamepambwa nafaka, Yanashangilia, na kuimba pamoja kwa shangwe.
Maana BWANA ameufariji Sayuni; amepafariji mahali pake palipokuwa ukiwa; amefanya nyika yake kuwa kama bustani ya Edeni, na jangwa lake kama bustani ya BWANA; shangwe na furaha zitaonekana ndani yake, kushukuru, na sauti ya kuimba.
Nami nitazidisha matunda ya miti, na mazao ya mashamba, msipate tena kutukanwa na mataifa kwa sababu ya njaa.
Nao watasema, Nchi hii, iliyokuwa ukiwa, imekuwa kama bustani ya Adeni; nayo miji iliyokuwa mahame, na ukiwa, na magofu, sasa ina maboma, inakaliwa na watu.
Lakini ninyi, enyi milima ya Israeli, mtachipuza matawi yenu na kuwapa watu wangu Israeli matunda yenu; maana wako karibu kuja.
na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya elfu mia moja na ishirini, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?
katika wakati huo wote, mtu alipofikia rundo la vipimo ishirini, palikuwa na vipimo kumi tu; na mtu alipofikia pipa kubwa apate kuteka divai ya vyombo hamsini, palikuwa na divai ya vyombo ishirini tu.
Kwa maana itakuwako mbegu ya amani; mzabibu utatoa matunda yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, na hizo mbingu zitatoa umande wake; nami nitawarithisha mabaki ya watu hawa vitu hivi vyote.