Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Yoeli 2:15 - Swahili Revised Union Version

Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu;

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Pigeni tarumbeta huko Siyoni! Toeni amri watu wafunge; itisheni mkutano wa kidini.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Pigeni tarumbeta huko Siyoni! Toeni amri watu wafunge; itisheni mkutano wa kidini.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Pigeni tarumbeta huko Siyoni! Toeni amri watu wafunge; itisheni mkutano wa kidini.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Pigeni tarumbeta katika Sayuni, tangazeni saumu takatifu, liiteni kusanyiko takatifu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Pigeni tarumbeta katika Sayuni, tangazeni saumu takatifu, liiteni kusanyiko takatifu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu;

Tazama sura
Tafsiri zingine

Yoeli 2:15
8 Marejeleo ya Msalaba  

Wakapiga mbiu ya watu kufunga, wakamweka Nabothi juu mbele ya watu.

Akaandika katika zile nyaraka, akasema, Pigeni mbiu ya watu kufunga, mkamketishe Nabothi juu mbele ya watu,

Yehu akasema, Takaseni kusanyiko la dini kwa Baali. Wakalitangaza.

Msilete tena matoleo ya ubatili; uvumba ni chukizo kwangu; mwezi mwandamo na sabato, kuita makutano; siyawezi maovu hayo na makutano ya ibada.

Basi, ikawa katika mwaka wa tano wa Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa tisa, watu wote waliokuwa katika Yerusalemu, na watu wote waliokuja Yerusalemu kutoka miji yote ya Yuda, wakapiga mbiu ya kufunga mbele za BWANA.

Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini, Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu, Na kumlilia BWANA,

Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; Wenyeji wote wa nchi na watetemeke; Kwa maana siku ya BWANA inakuja. Kwa sababu inakaribia;

Na hapo watakapozipiga hizo tarumbeta, mkutano wote utakukutanikia wewe, hapo mlangoni pa hema ya kukutania.