Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yoeli 1:9 - Swahili Revised Union Version

Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji Zimekatiliwa mbali na nyumba ya BWANA; Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, wanaomboleza.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Sadaka za nafaka na kinywaji zimetoweka nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu. Makuhani, wahudumu wa Mwenyezi-Mungu, wanaomboleza.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Sadaka za nafaka na kinywaji zimetoweka nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu. Makuhani, wahudumu wa Mwenyezi-Mungu, wanaomboleza.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Sadaka za nafaka na kinywaji zimetoweka nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu. Makuhani, wahudumu wa Mwenyezi-Mungu, wanaomboleza.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Sadaka za nafaka na sadaka za kinywaji zimekatiliwa mbali kutoka nyumba ya Mwenyezi Mungu. Makuhani wanaomboleza, wale wanaohudumu mbele za Mwenyezi Mungu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Sadaka za nafaka na sadaka za kinywaji zimekatiliwa mbali kutoka nyumba ya bwana. Makuhani wanaomboleza, wale wanaohudumu mbele za bwana.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji Zimekatiliwa mbali na nyumba ya BWANA; Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, wanaomboleza.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yoeli 1:9
10 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini sisi, BWANA ndiye Mungu wetu, wala sisi hatukumwacha; tena tunao makuhani wanaomtumikia BWANA, wana wa Haruni, na Walawi, kwa kazi yao;


Nawe umlete Haruni ndugu yako karibu nami, na wanawe pamoja naye, miongoni mwa wana wa Israeli, ili anitumikie katika kazi ya ukuhani. Haruni, na Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari, wana wa Haruni.


Bali ninyi mtaitwa makuhani wa BWANA; watu watawaiteni wahudumu wa Mungu wetu; mtakula utajiri wa mataifa, na kujisifia utukufu wao.


Mimi ninayalilia mambo hayo; Jicho langu, jicho langu linachuruzika machozi; Kwa kuwa mfariji yuko mbali nami, Ambaye ilimpasa kunihuisha nafsi; Watoto wangu wameachwa peke yao, Kwa sababu huyo adui ameshinda.


Njia za Sayuni zaomboleza, Kwa kuwa hakuna ajaye kwa sikukuu; Malango yake yote yamekuwa ukiwa, Makuhani wake hupiga kite; Wanawali wake wanahuzunika; Na yeye mwenyewe huona uchungu.


Hawatammiminia BWANA divai, wala hazitampendeza sadaka zao; mkate wao utakuwa kama chakula cha matanga kwao; wote watakaokila watatiwa unajisi; kwa maana mkate wao utakuwa kwa shauku zao; hautaingia katika nyumba ya BWANA.


Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani; Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu; Njooni mlale usiku kucha katika magunia, Enyi wahudumu wa Mungu wangu; Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji Zimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu.


Je! Chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu? Naam, furaha na kicheko mbali na nyumba ya Mungu wetu?


Ni nani ajuaye kwamba hatarudi na kugeuka, na kutuachia baraka nyuma yake, naam, sadaka ya unga, na sadaka ya kinywaji, kwa BWANA, Mungu wenu?


Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, na walie Kati ya patakatifu na madhabahu, Na waseme, Uwaachilie watu wako, Ee BWANA, Wala usiutoe urithi wako upate aibu, Hata mataifa watawale juu yao; Kwa nini waseme kati ya watu, Yuko wapi Mungu wao?