Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 61:6 - Swahili Revised Union Version

6 Bali ninyi mtaitwa makuhani wa BWANA; watu watawaiteni wahudumu wa Mungu wetu; mtakula utajiri wa mataifa, na kujisifia utukufu wao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Nanyi mtaitwa: “Makuhani wa Mwenyezi-Mungu”, Mtaitwa: “Watumishi wake Mungu wetu”. Mtafaidika kwa utajiri wa mataifa, mtatukuka kwa mali zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Nanyi mtaitwa: “Makuhani wa Mwenyezi-Mungu”, Mtaitwa: “Watumishi wake Mungu wetu”. Mtafaidika kwa utajiri wa mataifa, mtatukuka kwa mali zao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Nanyi mtaitwa: “Makuhani wa Mwenyezi-Mungu”, Mtaitwa: “Watumishi wake Mungu wetu”. Mtafaidika kwa utajiri wa mataifa, mtatukuka kwa mali zao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Nanyi mtaitwa makuhani wa Mwenyezi Mungu, mtaitwa watumishi wa Mungu wetu. Mtakula utajiri wa mataifa, nanyi katika utajiri wao mtajisifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Nanyi mtaitwa makuhani wa bwana, mtaitwa watumishi wa Mungu wetu. Mtakula utajiri wa mataifa, nanyi katika utajiri wao mtajisifu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 Bali ninyi mtaitwa makuhani wa BWANA; watu watawaiteni wahudumu wa Mungu wetu; mtakula utajiri wa mataifa, na kujisifia utukufu wao.

Tazama sura Nakili




Isaya 61:6
25 Marejeleo ya Msalaba  

nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli.


Na biashara yake na ujira wake utakuwa wakfu kwa BWANA, hautawekwa hazinani wala hautawekwa akiba; bali mapato ya biashara yake yatakuwa mali zao wakaao mbele za BWANA, wapate kula na kushiba, na kuvaa mavazi ya fahari.


Kwa maana utaenea upande wa kulia na upande wa kushoto; na wazao wako watawamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu.


Na wageni, walioandamana na BWANA ili wamhudumu, na kulipenda jina la BWANA, kuwa watumishi wake; kila aishikaye sabato asiivunje, na kulishika sana agano langu;


Maana BWANA asema hivi, Tazama, nitamwelekezea amani kama mto, na utukufu wa mataifa kama kijito kifurikacho, nanyi mtapata kunyonya; mtabebwa; na juu ya magoti mtabembelezwa.


Na baadhi ya hao nitawatwaa kuwa makuhani na Walawi, asema BWANA.


wala makuhani Walawi hawatakosa kuwa na mtu wa kusimama mbele zangu, na kutoa sadaka za kuteketezwa, na kufukiza matoleo, na kufanya dhabihu daima.


ili nyumba ya Israeli wasipotee mbali nami, wala wasijitie unajisi tena kwa makosa yao yote; bali wawe watu wangu, nami niwe Mungu wao, asema Bwana MUNGU.


Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.


Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa.


Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.


Wao ni wahudumu wa Kristo? (Nanena kiwazimu), mimi ni zaidi; katika taabu kuzidi sana; katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi.


bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; katika subira nyingi, katika mateso, katika shida, katika matatizo;


Wala wasiwe na urithi kati ya ndugu zao; BWANA ndiye urithi wao, kama alivyowaambia.


Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa muwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.


Bali ninyi ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;


na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina.


Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.


ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo