Yoeli 1:16 - Swahili Revised Union Version Je! Chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu? Naam, furaha na kicheko mbali na nyumba ya Mungu wetu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mazao yetu yameharibiwa huku tunatazama. Furaha na kicheko vimetoweka nyumbani kwa Mungu wetu. Biblia Habari Njema - BHND Mazao yetu yameharibiwa huku tunatazama. Furaha na kicheko vimetoweka nyumbani kwa Mungu wetu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mazao yetu yameharibiwa huku tunatazama. Furaha na kicheko vimetoweka nyumbani kwa Mungu wetu. Neno: Bibilia Takatifu Je, chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu: furaha na shangwe kutoka nyumba ya Mungu wetu? Neno: Maandiko Matakatifu Je, chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu: furaha na shangwe kutoka nyumba ya Mungu wetu? BIBLIA KISWAHILI Je! Chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu? Naam, furaha na kicheko mbali na nyumba ya Mungu wetu? |
Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu, kwa Mungu aliye furaha yangu na shangwe yangu; Nitakusifu kwa kinubi, Ee MUNGU, Mungu wangu.
basi, siku ile atainua sauti yake, akisema, Mimi sitakuwa mponya watu; kwa maana ndani ya nyumba yangu hamna chakula wala mavazi; wala hamtanifanya kuwa mtawala juu ya watu hawa.
Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani; Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu; Njooni mlale usiku kucha katika magunia, Enyi wahudumu wa Mungu wangu; Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji Zimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu.