Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Isaya 3:7 - Swahili Revised Union Version

7 basi, siku ile atainua sauti yake, akisema, Mimi sitakuwa mponya watu; kwa maana ndani ya nyumba yangu hamna chakula wala mavazi; wala hamtanifanya kuwa mtawala juu ya watu hawa.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Lakini siku hiyo atasema, “Mimi siwezi kuwa mwuguzi, nyumbani mwangu hamna chakula wala mavazi. Msinifanye mimi kuwa kiongozi wenu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Lakini siku hiyo atasema, “Mimi siwezi kuwa mwuguzi, nyumbani mwangu hamna chakula wala mavazi. Msinifanye mimi kuwa kiongozi wenu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Lakini siku hiyo atasema, “Mimi siwezi kuwa mwuguzi, nyumbani mwangu hamna chakula wala mavazi. Msinifanye mimi kuwa kiongozi wenu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Lakini siku hiyo atapiga kelele akisema, “Sina msaada. Sina chakula wala mavazi katika nyumba yangu, msinifanye niwe kiongozi wa watu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Lakini siku hiyo atapiga kelele akisema, “Sina uponyaji. Sina chakula wala mavazi katika nyumba yangu, msinifanye niwe kiongozi wa watu.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 basi, siku ile atainua sauti yake, akisema, Mimi sitakuwa mponya watu; kwa maana ndani ya nyumba yangu hamna chakula wala mavazi; wala hamtanifanya kuwa mtawala juu ya watu hawa.

Tazama sura Nakili

Isaya 3:7
10 Marejeleo ya Msalaba  

Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa BWANA, Mungu Aliye Juu sana, Muumba mbingu na nchi,

Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejesha njia za kukaa.

Je! Umemkataa Yuda kabisa? Roho yako imeichukia Sayuni? Mbona umetupiga, tusiwe na dawa ya kutuponya? Tulitazamia amani, lakini hayakuja mema yoyote, tulitazamia wakati wa kupona, na tazama, kufadhaika tu!

Nikushuhudie nini? Nikufananishe na nini, Ee Binti Yerusalemu? Nikulinganishe na nini, nipate kukufariji, Ee bikira binti Sayuni? Kwa maana uvunjifu wako ni mkuu kama bahari, Ni nani awezaye kukuponya?

Wagonjwa hamkuwatia nguvu, wala hamkuwaponya wenye maradhi, wala hamkuwafunga waliovunjika, wala hamkuwarudisha waliofukuzwa, wala hamkuwatafuta waliopotea; bali kwa nguvu na kwa ukali mmewatawala.

Efraimu alipouona ugonjwa wake, na Yuda jeraha lake, ndipo Efraimu alipokwenda kwa Ashuru, akatuma watu kwa mfalme Yarebu; lakini yeye hawezi kuwapoza, wala hatawaponya jeraha lenu.

Njooni, tumrudie BWANA; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga majeraha yetu.

Je! Chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu? Naam, furaha na kicheko mbali na nyumba ya Mungu wetu?

Maana, nainua mkono wangu mbinguni, Na kusema, Kama Mimi niishivyo milele,

Tufuate:

Matangazo

Matangazo