Yakobo 1:24 - Swahili Revised Union Version Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hujiangalia mwenyewe, kisha huenda zake, na mara husahau jinsi alivyo. Biblia Habari Njema - BHND Hujiangalia mwenyewe, kisha huenda zake, na mara husahau jinsi alivyo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hujiangalia mwenyewe, kisha huenda zake, na mara husahau jinsi alivyo. Neno: Bibilia Takatifu na baada ya kujiona alivyo, huenda zake na husahau upesi jinsi alivyo. Neno: Maandiko Matakatifu na baada ya kujiona alivyo, huenda zake na mara husahau jinsi alivyo. BIBLIA KISWAHILI Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. |
Na wote walioyasikia wakayaweka mioyoni mwao, wakisema, Mtoto huyu atakuwa wa namna gani? Kwa sababu mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.
Basi, yule Farisayo aliyemwalika alipoona vile, alisema moyoni mwake, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angemtambua mwanamke huyu amgusaye, ni nani, naye ni wa namna gani, ya kwamba ni mwenye dhambi.
ya kwamba Injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.
Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.
Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.
Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa,
Ndipo akawaambia hao Zeba na Salmuna, Hao watu mliowaua huko Tabori walikuwa watu wa namna gani? Wakamjibu, Walikuwa kama wewe ulivyo; kila mmoja alikuwa anafanana na wana wa mfalme.