Nao watumishi wa Absalomu wakamwendea yule mwanamke mle nyumbani; wakasema, Wako wapi Yonathani na Ahimaasi? Yule mwanamke akawaambia, Wamevuka kijito cha maji. Basi walipokwisha kuwatafuta wasiwaone, wakarudi Yerusalemu.
Walawi 19:11 - Swahili Revised Union Version Msiibe, wala msidanganye, wala msiambiane uongo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Msiibe, msidanganye wala kuambiana uongo. Biblia Habari Njema - BHND “Msiibe, msidanganye wala kuambiana uongo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Msiibe, msidanganye wala kuambiana uongo. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Usiibe. “ ‘Usiseme uongo. “ ‘Msidanganyane. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Usiibe. “ ‘Usiseme uongo. “ ‘Msidanganyane. BIBLIA KISWAHILI Msiibe, wala msidanganye, wala msiambiane uongo. |
Nao watumishi wa Absalomu wakamwendea yule mwanamke mle nyumbani; wakasema, Wako wapi Yonathani na Ahimaasi? Yule mwanamke akawaambia, Wamevuka kijito cha maji. Basi walipokwisha kuwatafuta wasiwaone, wakarudi Yerusalemu.
Akamwambia, Mimi nami ni nabii kama wewe, na malaika akaniambia kwa neno la BWANA, kusema, Mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo.
Hatakaa ndani ya nyumba yangu Mtu atendaye hila. Asemaye uongo hatathibitika Mbele ya macho yangu.
Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala chochote alicho nacho jirani yako.
Mtu akiiba ng'ombe au kondoo, na kumchinja, au kumwuza; atalipa ng'ombe watano badala ya ng'ombe mmoja, na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja.
Mtu akimpa mwenziwe amana ya fedha au vitu vingine amtunzie, na vitu vile vikaibwa katika nyumba ya mtu huyo; mwizi akipatikana, atalipa thamani yake mara mbili.
Kwa maana, tangu aliye mdogo hata aliye mkubwa miongoni mwao, kila mmoja ni mtamanifu; na, tangu nabii hata kuhani, kila mmoja hutenda mambo ya udanganyifu.
wala usiyakusanye masazo ya mizabibu yako, wala usiyaokote matunda ya mizabibu yako yaliyopukutika; uyaache kwa ajili ya maskini na mgeni; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
La hasha! Mungu aonekane kuwa kweli japo kila mtu ni mwongo; kama ilivyoandikwa, Ili ujulikane kuwa una haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu.
Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake.
Mwizi asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akifanya kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.
na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na linginelo lolote lisilopatana na mafundisho ya kweli;
Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.