Ikawa matoleo yake ni sadaka ya kuteketezwa ya ng'ombe, atatoa ng'ombe dume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya BWANA.
Walawi 16:7 - Swahili Revised Union Version Kisha atawatwaa wale mbuzi wawili na kuwaweka mbele za BWANA mlangoni pa hema ya kukutania. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha, wale beberu wawili atawaweka kwenye mlango wa hema la mkutano. Biblia Habari Njema - BHND Kisha, wale beberu wawili atawaweka kwenye mlango wa hema la mkutano. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha, wale beberu wawili atawaweka kwenye mlango wa hema la mkutano. Neno: Bibilia Takatifu Kisha atawachukua wale beberu wawili na kuwaleta mbele za Mwenyezi Mungu kwenye ingilio la Hema la Kukutania. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha atawachukua wale mbuzi dume wawili na kuwaleta mbele za bwana kwenye ingilio la Hema la Kukutania. BIBLIA KISWAHILI Kisha atawatwaa wale mbuzi wawili na kuwaweka mbele za BWANA mlangoni pa hema ya kukutania. |
Ikawa matoleo yake ni sadaka ya kuteketezwa ya ng'ombe, atatoa ng'ombe dume mkamilifu; ataleta mlangoni pa hema ya kukutania, ili akubaliwe mbele ya BWANA.
Na Haruni atamtoa yule ng'ombe wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya nafsi yake, na kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake.
Na Haruni atapiga kura juu ya wale mbuzi wawili; kura moja kwa ajili ya BWANA; na kura ya pili kwa ajili ya Azazeli.
Naye atamleta huyo ng'ombe na kumweka mlangoni pa hiyo hema ya kukutania, mbele za BWANA; naye ataweka mkono wake kichwani mwake ng'ombe, na kumchinja huyo ng'ombe mbele za BWANA.
Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.
Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.