Naye Isaya akasema, Twaeni mkate wa tini. Wakautwaa, wakauweka juu ya jipu, naye akapona.
Walawi 13:18 - Swahili Revised Union Version Tena mwili wa mtu utakapokuwa na jipu katika ngozi yake, nalo limepoa, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Kama mtu ameshikwa na jipu, nalo limepona, Biblia Habari Njema - BHND “Kama mtu ameshikwa na jipu, nalo limepona, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Kama mtu ameshikwa na jipu, nalo limepona, Neno: Bibilia Takatifu “Wakati mtu ana jipu juu ya ngozi yake nalo likapona, Neno: Maandiko Matakatifu “Wakati mtu ana jipu juu ya ngozi yake nalo likapona, BIBLIA KISWAHILI Tena mwili wa mtu utakapokuwa na jipu katika ngozi yake, nalo limepoa, |
Naye Isaya akasema, Twaeni mkate wa tini. Wakautwaa, wakauweka juu ya jipu, naye akapona.
Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA, akampiga Ayubu na majipu mabaya tangu wayo wa mguu hadi utosi wa kichwa.
akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yoyote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi BWANA nikuponyaye.
Nayo yatakuwa ni mavumbi membamba juu ya nchi yote ya Misri, nayo yatakuwa majipu yenye kufura na kutumbuka juu ya wanadamu na juu ya wanyama, katika nchi yote ya Misri.
na huyo kuhani atamwangalia; ikiwa hilo pigo limegeuzwa kuwa jeupe, ndipo huyo kuhani atasema kuwa huyo aliyekuwa na pigo ni safi.
na mahali palipokuwa na lile jipu pana uvimbe mweupe, au kipaku king'aacho, cheupe lakini chekundu kidogo, ndipo atamwonesha kuhani mahali hapo;
ndipo kuhani atapaangalia; ikiwa nywele iliyo katika kile kipaku imegeuka kuwa nyeupe, na kwamba kumeonekana kuingia ndani kuliko ngozi yenyewe; ni ukoma, umetokea katika mahali palipoungua; na kuhani atasema kuwa ni najisi; hili ni pigo la ukoma.