Basi kwa siku nyingi Israeli wamekuwa hawana Mungu wa kweli, wala hawana kuhani afundishaye, wala hawana torati;
Walawi 10:11 - Swahili Revised Union Version tena mpate kuwafundisha wana wa Israeli amri hizi zote ambazo BWANA amewaambia kwa mkono wa Musa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtawafundisha Waisraeli masharti yote ambayo nimewaambia kwa njia ya Mose.” Biblia Habari Njema - BHND Mtawafundisha Waisraeli masharti yote ambayo nimewaambia kwa njia ya Mose.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtawafundisha Waisraeli masharti yote ambayo nimewaambia kwa njia ya Mose.” Neno: Bibilia Takatifu na lazima mwafundishe Waisraeli amri zote ambazo Mwenyezi Mungu aliwapa kupitia Musa.” Neno: Maandiko Matakatifu na lazima mwafundishe Waisraeli amri zote ambazo bwana aliwapa kupitia Musa.” BIBLIA KISWAHILI tena mpate kuwafundisha wana wa Israeli amri hizi zote ambazo BWANA amewaambia kwa mkono wa Musa. |
Basi kwa siku nyingi Israeli wamekuwa hawana Mungu wa kweli, wala hawana kuhani afundishaye, wala hawana torati;
Wakafundisha katika Yuda, wenye kitabu cha Torati ya BWANA; wakazunguka katika miji yote ya Yuda, wakafundisha kati ya watu.
Hezekia akawafurahisha mioyo Walawi wote waliokuwa mastadi wa kumtumikia BWANA. Basi muda wa siku saba wakala sikukuu, wakitoa dhabihu za sadaka za amani, na kumtolea shukrani BWANA, Mungu wa baba zao.
Naye Ezra, kuhani, akaileta Torati mbele ya mkutano mzima, wanaume na wanawake, na wote walioweza kusikia na kufahamu, siku ya kwanza na mwezi wa saba.
Nao wakasoma katika kitabu, katika Torati ya Mungu, kwa sauti ya kusikika; wakaeleza maana yake, hata wakayafahamu yaliyosomwa.
Hapo ndipo waliposema, Njooni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njooni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno yake yoyote.
Makuhani hawakusema, Yuko wapi BWANA? Wala wanasheria hawakunijua; wachungaji nao waliniasi, nao manabii walitoa unabii kwa Baali, wakafuata mambo yasiyofaidia kitu.
Kwa maana yapasa midomo ya kuhani ihifadhi maarifa, tena yawapasa watu kuitafuta sheria kinywani mwake; kwa kuwa yeye ni mjumbe wa BWANA wa majeshi.
na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
nawe fanya sawasawa na hukumu watakayokuonesha mahali hapo atakapochagua BWANA; nawe tunza kufanya kwa mfano wa yote watakayokufunza;
kwa mfano wa sheria watakayokufunza, na kwa mfano wa hukumu watakayokuambia, fanya vivyo hivyo; usigeuke katika hukumu watakayokuonesha, kwenda mkono wa kulia wala wa kushoto.
Angalia katika pigo la ukoma, utunze kwa bidii, kwa kufanya mfano wa yote watakayowafundisha makuhani Walawi; tunzeni kwa kuyafanya vile vile kama nilivyowaamuru wao.
Watamfundisha Yakobo hukumu zako, Na Israeli torati yako, Wataweka uvumba mbele zako, Na sadaka nzima za kuteketezwa madhabahuni mwako.