Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliyokwisha kuchongwa machimboni; wala nyundo, wala shoka, wala chombo cha chuma chochote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba.
Waefeso 2:21 - Swahili Revised Union Version Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yeye ndiye mwenye kuliunganisha jengo lote na kulikuza hata liwe hekalu takatifu kwa ajili ya Bwana. Biblia Habari Njema - BHND Yeye ndiye mwenye kuliunganisha jengo lote na kulikuza hata liwe hekalu takatifu kwa ajili ya Bwana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yeye ndiye mwenye kuliunganisha jengo lote na kulikuza hata liwe hekalu takatifu kwa ajili ya Bwana. Neno: Bibilia Takatifu Ndani yake jengo lote limeshikamanishwa pamoja na kuinuliwa ili kuwa Hekalu takatifu katika Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Ndani yake jengo lote limeshikamanishwa pamoja na kusimamishwa ili kuwa Hekalu takatifu katika Bwana Mwenyezi. BIBLIA KISWAHILI Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. |
Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliyokwisha kuchongwa machimboni; wala nyundo, wala shoka, wala chombo cha chuma chochote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba.
Shuhuda zako ni amini sana; Utakatifu ndio uifaao nyumba yako, Ee BWANA, milele na milele.
Na sawasawa na milango ya vyumba, vilivyoelekea upande wa kusini, palikuwa na mlango katika mwisho wa njia ile; yaani, njia iliyoukabili ukuta upande wa mashariki, mtu akiingia.
Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.
Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
wala hakishiki Kichwa, ambacho kwa yeye mwili wote ukineemeshwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kama atakavyo Mungu.
Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.