Nanyi twaeni tawi la hisopo, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu yeyote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi.
Waebrania 9:18 - Swahili Revised Union Version Kwa hiyo hata lile la kwanza halikuanzwa pasipo damu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ndiyo maana hata lile agano la kwanza halikuwekwa bila damu kumwagwa. Biblia Habari Njema - BHND Ndiyo maana hata lile agano la kwanza halikuwekwa bila damu kumwagwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ndiyo maana hata lile agano la kwanza halikuwekwa bila damu kumwagwa. Neno: Bibilia Takatifu Hii ndiyo sababu hata lile agano la kwanza halikuweza kutekelezwa pasipo damu. Neno: Maandiko Matakatifu Hii ndiyo sababu hata lile agano la kwanza halikuweza kutekelezwa pasipo damu. BIBLIA KISWAHILI Kwa hiyo hata lile la kwanza halikuanzwa pasipo damu. |
Nanyi twaeni tawi la hisopo, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu yeyote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi.
Kisha akawaleta wana wa Haruni, na Musa akaitia hiyo damu katika ncha za masikio ya upande wa kulia, na katika vidole vya gumba vya mikono yao ya kulia, na katika vidole vya gumba vya maguu yao ya kulia; kisha Musa akainyunyiza hiyo damu katika madhabahu pande zote.
basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na dosari, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?
Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya.
Maana kila amri ilipokwisha kunenwa na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu chenyewe, na watu wote,
Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.