Waebrania 3:13 - Swahili Revised Union Version Lakini mwonyane kila siku, maadamu inaitwa leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maadamu hiyo “Leo” inayosemwa katika Maandiko bado inatuhusu sisi, mnapaswa kusaidiana daima, ili mtu yeyote miongoni mwenu asidanganywe na dhambi na kuwa mkaidi. Biblia Habari Njema - BHND Maadamu hiyo “Leo” inayosemwa katika Maandiko bado inatuhusu sisi, mnapaswa kusaidiana daima, ili mtu yeyote miongoni mwenu asidanganywe na dhambi na kuwa mkaidi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maadamu hiyo “Leo” inayosemwa katika Maandiko bado inatuhusu sisi, mnapaswa kusaidiana daima, ili mtu yeyote miongoni mwenu asidanganywe na dhambi na kuwa mkaidi. Neno: Bibilia Takatifu Lakini mtiane moyo mtu na mwenzake kila siku, maadamu inaitwa “Leo”, ili asiwepo hata mmoja wenu mwenye kufanywa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini mtiane moyo mtu na mwenzake kila siku, maadamu iitwapo Leo, ili asiwepo hata mmoja wenu mwenye kufanywa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. BIBLIA KISWAHILI Lakini mwonyane kila siku, maadamu inaitwa leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. |
Hula majivu; moyo uliodanganyika umempotosha, asiweze kuiokoa nafsi yake, wala kusema, Je! Sio uongo mkononi mwangu?
Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Mwenye makao yako juu sana; Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi?
Naye, alipofika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa moyo wote.
mvue mwenendo wenu wa kwanza, utu wa zamani unaoharibika, kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya;
vile vile, kama mjuavyo, jinsi tulivyomwonya kila mmoja wenu kama baba awaonyavyo watoto wake mwenyewe, tukiwatia moyo na kushuhudia;
lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.
Lakini nawasihi, ndugu, mchukuliane na neno hili lenye maonyo maana nimewaandikia kwa maneno machache.