Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Obadia 1:3 - Swahili Revised Union Version

3 Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Mwenye makao yako juu sana; Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Kiburi chako kimekudanganya: Kwa kuwa mji wako mkuu ni ngome ya miamba imara na makao yako yapo juu milimani, hivyo wajisemea, ‘Nani awezaye kunishusha chini?’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Kiburi chako kimekudanganya: Kwa kuwa mji wako mkuu ni ngome ya miamba imara na makao yako yapo juu milimani, hivyo wajisemea, ‘Nani awezaye kunishusha chini?’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Kiburi chako kimekudanganya: kwa kuwa mji wako mkuu ni ngome ya miamba imara na makao yako yapo juu milimani, hivyo wajisemea, ‘Nani awezaye kunishusha chini?’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, wewe unayeishi katika mapango ya miamba na kufanya makao yako juu, wewe unayejiambia mwenyewe, ‘Ni nani awezaye kunishusha chini?’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, wewe unayeishi katika majabali ya miamba na kufanya makao yako juu, wewe unayejiambia mwenyewe, ‘Ni nani awezaye kunishusha chini?’

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika mapango ya majabali, Mwenye makao yako juu sana; Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi?

Tazama sura Nakili




Obadia 1:3
21 Marejeleo ya Msalaba  

Esau akakaa katika mlima Seiri, Esau ndiye Edomu.


Akawaua Waedomi katika Bonde la Chumvi watu elfu kumi; akautwaa Sela vitani, akauita jina lake Yoktheeli hata leo.


Amazia akapiga moyo konde, akawaongoza watu wake, akaenda mpaka Bonde la Chumvi, akawapiga katika wana wa Seiri watu elfu kumi.


Na elfu kumi wengine, ambao wana wa Yuda waliwachukua wakiwa hai, wakawaleta juu ya jabali, wakawaangusha chini toka juu ya jabali, hadi wakavunjikavunjika wote.


Ujapopanda ukuu wake mpaka mbinguni, Na kichwa chake kufikia mawinguni;


Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.


Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.


Kiburi cha mtu kitamshusha; Bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa.


Tumesikia habari za kiburi cha Moabu, ya kwamba ni mwenye kiburi kingi; habari za majivuno yake, na kiburi chake, na ghadhabu yake; majivuno yake si kitu.


Tazama, mimi niko juu yako, Ewe ukaaye bondeni, na kwenye jabali la uwandani, asema BWANA ninyi mnaosema, Ni nani atakayeshuka apigane nasi? Au, Ni nani atakayeingia katika makao yetu?


BWANA asema hivi, Msijidanganye mkisema, Bila shaka Wakaldayo watatuacha na kwenda zao; maana hawatawaacha.


Enyi mkaao Moabu, ondokeni mijini, Nendeni mkakae majabalini; Mkawe kama njiwa atengenezaye kiota chake Kandoni mwa mdomo wa shimo.


Kuhusu kuogofya kwako, Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Ushikaye kilele cha milima; Ujapofanya kiota chako juu sana kama tai, Nitakushusha kutoka huko; asema BWANA.


Mbona unajisifu kwa sababu ya mabonde, bonde lako litiririkalo, Ee binti mwenye kuasi? Utumainiaye hazina zako, ukisema, Ni nani atakayenijia?


Kwa wingi wa uchuuzi wako watu walikujaza udhalimu ndani yako, nawe umetenda dhambi; kwa sababu hiyo nimekutoa kwa nguvu katika mlima wa Mungu, kama kitu kilicho najisi; nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto.


Ijapokuwa Edomu asema, Tumepondwapondwa, lakini tutarudi na kupajenga mahali palipoachwa hali ya ukiwa; BWANA wa majeshi asema hivi, Wao watajenga, bali mimi nitaangusha; na watu watawaita, Mpaka wa uovu, na, Watu ambao BWANA anawaghadhabikia milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo