Waebrania 12:21 - Swahili Revised Union Version Na hayo yaliyoonekana jinsi yalivyokuwa ya kutisha, hata Musa akasema, Nimeshikwa na hofu na kutetemeka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hayo yote yalionekana ya kutisha mno, hata Mose akasema, “Naogopa na kutetemeka.” Biblia Habari Njema - BHND Hayo yote yalionekana ya kutisha mno, hata Mose akasema, “Naogopa na kutetemeka.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hayo yote yalionekana ya kutisha mno, hata Mose akasema, “Naogopa na kutetemeka.” Neno: Bibilia Takatifu Waliyoyaona yalikuwa ya kutisha kiasi kwamba Musa alisema, “Ninatetemeka kwa hofu.” Neno: Maandiko Matakatifu Waliyoyaona yalikuwa ya kutisha kiasi kwamba Musa alisema, “Ninatetemeka kwa hofu.” BIBLIA KISWAHILI Na hayo yaliyoonekana jinsi yalivyokuwa ya kutisha, hata Musa akasema, Nimeshikwa na hofu na kutetemeka. |
Ikawa siku ya tatu, wakati wa asubuhi, palikuwa na ngurumo na umeme, na wingu zito juu ya mlima, na sauti ya baragumu iliyolia sana. Watu wote waliokuwa kituoni wakatetemeka.
Na hapo sauti ya baragumu ilipozidi kulia sana, Musa akanena, naye Mungu akamwitikia kwa sauti.
Maana, mtumishi wa Bwana wangu huyu atawezaje kusema na Bwana wangu huyu? Kwa maana kwangu mimi, mara hazikusalia nguvu ndani yangu, wala pumzi haikusalia ndani yangu.
Basi nikaachwa peke yangu, nikaona maono haya makubwa, wala hazikubaki nguvu ndani yangu; maana uzuri wangu uligeuzwa ndani yangu kuwa uharibifu, wala sikubakiziwa nguvu.
Kwa kuwa niliogopa hasira na makamio aliyowakasirikia BWANA kutaka kuwaangamiza. Lakini BWANA alinisikiza wakati huo nao.
bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.
Nami nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kulia juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,