Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 10:17 - Swahili Revised Union Version

17 Maana, mtumishi wa Bwana wangu huyu atawezaje kusema na Bwana wangu huyu? Kwa maana kwangu mimi, mara hazikusalia nguvu ndani yangu, wala pumzi haikusalia ndani yangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Mimi ni kama mtumwa mbele ya bwana wake. Nawezaje kuzungumza nawe? Sina nguvu na pumzi imeniishia!’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Mimi ni kama mtumwa mbele ya bwana wake. Nawezaje kuzungumza nawe? Sina nguvu na pumzi imeniishia!’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Mimi ni kama mtumwa mbele ya bwana wake. Nawezaje kuzungumza nawe? Sina nguvu na pumzi imeniishia!’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Bwana wangu, mimi mtumishi wako nitawezaje kuzungumza na wewe? Nguvu zangu zimeniishia, hata ninashindwa kupumua.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Bwana wangu, mimi mtumishi wako nitawezaje kuzungumza na wewe? Nguvu zangu zimeniishia hata ninashindwa kupumua.”

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

17 Mimi niliye mtumwa wa Bwana wangu nitawezaje kusema na wewe uliye Bwana wangu? Kwani kwangu mimi hakuna nguvu zilizoko bado, wala pumzi haikusalia mwangu.

Tazama sura Nakili




Danieli 10:17
11 Marejeleo ya Msalaba  

Tena semeni, Tazama, mtumwa wako, Yakobo, yuko nyuma yetu. Maana alisema, Nitamsuluhisha kwa zawadi inayonitangulia, baadaye nitamwona uso wake; huenda atanikubali uso wangu.


Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi.


Basi nikaachwa peke yangu, nikaona maono haya makubwa, wala hazikubaki nguvu ndani yangu; maana uzuri wangu uligeuzwa ndani yangu kuwa uharibifu, wala sikubakiziwa nguvu.


Ndipo Danieli, aliyeitwa jina lake Belteshaza, akashangaa kwa muda, na fikira zake zikamfadhaisha. Mfalme akajibu akasema, Ee Belteshaza, ndoto ile isikufadhaishe wala tafsiri yake. Belteshaza akajibu, akasema, Bwana wangu, ndoto hii iwapate wao wakuchukiao, na tafsiri yake iwapate adui zako.


Daudi mwenyewe alisema, kwa uweza wa Roho Mtakatifu, Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kulia, Hata niwawekapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.


Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.


Gideoni akaona ya kuwa ni malaika wa BWANA; Gideoni akasema, Ole wangu, Ee Bwana MUNGU! Kwa kuwa nimemwona BWANA uso kwa uso.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo