Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.
Waebrania 11:15 - Swahili Revised Union Version Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurudi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama wangalikuwa wanaifikiria nchi walikotoka zamani, wangalipata nafasi ya kurudi huko. Biblia Habari Njema - BHND Kama wangalikuwa wanaifikiria nchi walikotoka zamani, wangalipata nafasi ya kurudi huko. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama wangalikuwa wanaifikiria nchi walikotoka zamani, wangalipata nafasi ya kurudi huko. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kweli kama wangekuwa wanafikiri kuhusu nchi waliyoiacha, wangepata nafasi ya kurudi huko. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kweli kama wangekuwa wanafikiri kuhusu nchi waliyoiacha, wangalipata nafasi ya kurudi huko. BIBLIA KISWAHILI Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurudi. |
Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.
Basi kulikuwa na njaa katika nchi ile; Abramu akashuka Misri, akae huko kwa muda maana njaa ilikuwa kali katika nchi.
Akachukua wanyama wake wote, na mali yake yote aliyokuwa amepata, na wanyama aliowapata katika Padan-aramu, ili afike kwa Isaka babaye katika nchi ya Kanaani.