Na hao watakaopanga upande wa mashariki, kwa kuelekea maawio ya jua, ndio wale wa bendera ya kambi ya Yuda, kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Yuda atakuwa Nashoni mwana wa Aminadabu.
Waamuzi 1:2 - Swahili Revised Union Version BWANA akasema, Yuda atakwea; tazama, nimeitia hiyo nchi mkononi mwake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu akawajibu, “Kabila la Yuda litakwenda kupigana nao kwanza, maana nimeitia nchi hiyo mikononi mwao.” Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu akawajibu, “Kabila la Yuda litakwenda kupigana nao kwanza, maana nimeitia nchi hiyo mikononi mwao.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu akawajibu, “Kabila la Yuda litakwenda kupigana nao kwanza, maana nimeitia nchi hiyo mikononi mwao.” Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu akajibu, “Yuda ndiye atakayetangulia; nimewapa hiyo nchi mikononi mwao.” Neno: Maandiko Matakatifu bwana akajibu, “Yuda ndiye atakayetangulia; nimewapa hiyo nchi mikononi mwao.” BIBLIA KISWAHILI BWANA akasema, Yuda atakwea; tazama, nimeitia hiyo nchi mkononi mwake. |
Na hao watakaopanga upande wa mashariki, kwa kuelekea maawio ya jua, ndio wale wa bendera ya kambi ya Yuda, kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Yuda atakuwa Nashoni mwana wa Aminadabu.
Basi aliyetoa matoleo yake siku ya kwanza ni Nashoni mwana wa Aminadabu, wa kabila la Yuda;
Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambalo Musa hakunena neno lolote juu yake katika mambo ya ukuhani.
Wakamwambia Yoshua, Hakika BWANA ameitia nchi yote katika mikono yetu; tena zaidi ya hayo wenyeji wa nchi wanayeyuka mbele yetu.
Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila la Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na ile mihuri yake saba.
Ndipo Yuda akamwambia Simeoni ndugu yake, Kwea wewe pamoja nami katika eneo langu, ili tupate kupigana na Wakanaani; kisha mimi nami nitakwenda pamoja nawe katika eneo lako. Basi Simeoni akaenda pamoja naye.
Basi wana wa Israeli wakainuka, wakakwea kwenda Betheli, nao wakataka shauri kwa Mungu; wakasema, Ni nani atakayekwea kwenda vitani kwanza kwa ajili yetu juu ya wana wa Benyamini? BWANA akawaambia, Yuda atakwea kwanza.
na Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni, alikuwa anasimama mbele ya hilo sanduku siku hizo), wakasema, Je! Nitoke tena niende kupigana na wana wa Benyamini ndugu yangu, au niache? BWANA akawaambia, Haya, kweeni; kwa kuwa kesho nitamtoa na kumtia mkononi mwako.