Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Waamuzi 1:3 - Swahili Revised Union Version

3 Ndipo Yuda akamwambia Simeoni ndugu yake, Kwea wewe pamoja nami katika eneo langu, ili tupate kupigana na Wakanaani; kisha mimi nami nitakwenda pamoja nawe katika eneo lako. Basi Simeoni akaenda pamoja naye.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Watu wa kabila la Yuda wakawaambia ndugu zao, watu wa kabila la Simeoni, “Shirikianeni nasi tunapokwenda kuitwaa nchi hiyo ambayo tumepewa. Nasi, pia tutashirikiana nanyi kwenda kuitwaa nchi mtakayopewa.” Hivyo kabila la Simeoni likakubali kushirikiana nao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Watu wa kabila la Yuda wakawaambia ndugu zao, watu wa kabila la Simeoni, “Shirikianeni nasi tunapokwenda kuitwaa nchi hiyo ambayo tumepewa. Nasi, pia tutashirikiana nanyi kwenda kuitwaa nchi mtakayopewa.” Hivyo kabila la Simeoni likakubali kushirikiana nao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Ndipo wanaume wa Yuda wakawaambia Wasimeoni ndugu zao, “Pandeni pamoja nasi katika nchi tuliyopewa, ili tupate kupigana na Wakanaani. Sisi pia tutaenda pamoja nanyi katika sehemu yenu mliyopewa.” Basi Wasimeoni wakaenda pamoja nao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Ndipo watu wa Yuda wakawaambia Wasimeoni ndugu zao, “Pandeni pamoja nasi katika nchi tuliyopewa, ili tupate kupigana na Wakanaani. Sisi pia tutakwenda pamoja nanyi katika sehemu yenu mliyopewa.” Basi Wasimeoni wakaenda pamoja nao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Ndipo Yuda akamwambia Simeoni ndugu yake, Kwea wewe pamoja nami katika eneo langu, ili tupate kupigana na Wakanaani; kisha mimi nami nitakwenda pamoja nawe katika eneo lako. Basi Simeoni akaenda pamoja naye.

Tazama sura Nakili

Waamuzi 1:3
7 Marejeleo ya Msalaba  

Akapata mimba tena akazaa mwana, akasema, Kwa kuwa BWANA amesikia ya kwamba mimi sikupendwa, amenipa na huyu; akamwita jina lake Simeoni.

Akasema, Wakiwa Washami hodari mno kwangu, ndipo wewe utanisaidia, lakini Waamoni wakiwa ni hodari mno kwako, ndipo mimi nitakuja nikusaidie wewe.

Kisha sehemu ya pili ilitokea kwa ajili ya Simeoni, maana, kwa ajili ya hilo kabila la wana wa Simeoni, kwa kufuata jamaa zao; na urithi wao ulikuwa katikati ya urithi wa wana wa Yuda.

Wa kabila la Simeoni elfu kumi na mbili. Wa kabila la Lawi elfu kumi na mbili. Wa kabila la Isakari elfu kumi na mbili.

Kisha Yuda akaenda pamoja na nduguye Simeoni, na wakawapiga Wakanaani waliokaa katika Sefathi, na kuuharibu mji kabisa. Na jina la mji huo ulikuwa ukiitwa Horma.

BWANA akasema, Yuda atakwea; tazama, nimeitia hiyo nchi mkononi mwake.

Yuda akakwea; naye BWANA akawatia Wakanaani na Waperizi mkononi mwao; nao wakawapiga huko Bezeki watu elfu kumi.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo