Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoshua 2:24 - Swahili Revised Union Version

24 Wakamwambia Yoshua, Hakika BWANA ameitia nchi yote katika mikono yetu; tena zaidi ya hayo wenyeji wa nchi wanayeyuka mbele yetu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Wakamwambia “Hakika Mwenyezi-Mungu ameitia nchi yote mikononi mwetu. Tena wakazi wa nchi hiyo wamekufa moyo kwa sababu yetu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Wakamwambia “Hakika Mwenyezi-Mungu ameitia nchi yote mikononi mwetu. Tena wakazi wa nchi hiyo wamekufa moyo kwa sababu yetu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Wakamwambia “Hakika Mwenyezi-Mungu ameitia nchi yote mikononi mwetu. Tena wakazi wa nchi hiyo wamekufa moyo kwa sababu yetu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Wakamwambia Yoshua, “Hakika Mwenyezi Mungu ametupatia nchi yote mikononi mwetu; watu wote wanayeyuka kwa hofu kwa sababu yetu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Wakamwambia Yoshua, “Hakika bwana ametupa nchi yote mikononi mwetu; watu wote wanayeyuka kwa hofu kwa sababu yetu.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

24 Wakamwambia Yoshua, Hakika BWANA ameitia nchi yote katika mikono yetu; tena zaidi ya hayo wenyeji wa nchi wanayeyuka mbele yetu.

Tazama sura Nakili




Yoshua 2:24
16 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo majumbe wa Edomu wakashangaa, Watu wa Moabu wenye nguvu tetemeko limewapata, Watu wote wakaao Kanaani wameyeyuka.


Nami nitakuwekea mpaka wako tangu Bahari ya Shamu hadi bahari ya Wafilisti, tena tangu jangwani hata huo Mto; kwa kuwa nitawatia wenyeji wa nchi mkononi mwako; nawe utawafukuza mbele yako.


Kama baridi ya theluji wakati wa mavuno; Ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwao wamtumao; Kwa maana huwaburudisha bwana zake nafsi zao.


Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda kulingana na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.


Kisha wale watu wakarudi, wakateremka mlimani, wakavuka, wakamwendea Yoshua, mwana wa Nuni, nao wakamwambia habari za mambo yote yaliyowapata.


Ikawa, wafalme wa Waamori, waliokaa ng'ambo ya Yordani pande za magharibi, na wafalme wote wa Wakanaani, waliokuwa karibu na bahari, waliposikia jinsi BWANA alivyoyakausha maji ya Yordani mbele ya wana wa Israeli, hadi tulipokwisha kuvuka, basi mioyo yao iliyeyuka, wala haikuwamo roho ya nguvu ndani yao tena; kwa ajili ya wana wa Israeli.


BWANA akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake, na mashujaa wake.


Kisha BWANA akamwambia Yoshua, Usiogope, wala usifadhaike; wachukue wanajeshi wako wote waende pamoja nawe, nanyi inukeni, mwende Ai, angalia, mimi nimemtia mkononi mwako huyo mfalme wa Ai, na watu wake, na mji wake, na nchi yake;


BWANA akasema, Yuda atakwea; tazama, nimeitia hiyo nchi mkononi mwake.


Hapo mtakapokwenda mtawafikia watu wakaao kwa amani, na hiyo nchi nayo ni kubwa; kwa kuwa Mungu ameitia mikononi mwenu; ni mahali ambapo hapapungukiwi na kitu chochote kilichoko duniani.


Ikawa usiku uo huo BWANA akamwambia, Ondoka, shuka kambini; maana nimeitia katika mikono yako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo