Basi Hilkia kuhani, na Ahikamu, na Akbori, na Shafani, na Asaya, wakamwendea Hulda, nabii wa kike, mkewe Shalumu, mwana wa Tikva, mwana wa Harhasi, mtunza mavazi ya mfalme; (naye alikaa Yerusalemu katika mtaa wa pili;) wakasema naye.
Nehemia 7:72 - Swahili Revised Union Version Na mabaki ya watu wakatoa darkoni za dhahabu elfu ishirini, na mane za fedha elfu mbili, na mavazi ya makuhani sitini na saba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Matoleo ya watu wengine wote yalikuwa kilo 168 za dhahabu, kilo 140 za fedha na mavazi ya makuhani 67. Biblia Habari Njema - BHND Matoleo ya watu wengine wote yalikuwa kilo 168 za dhahabu, kilo 140 za fedha na mavazi ya makuhani 67. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Matoleo ya watu wengine wote yalikuwa kilo 168 za dhahabu, kilo 140 za fedha na mavazi ya makuhani 67. Neno: Bibilia Takatifu Jumla ya matoleo ya watu wengine yalikuwa ni darkoni elfu ishirini za dhahabu, mane elfu mbili za fedha, na mavazi sitini na saba ya makuhani. Neno: Maandiko Matakatifu Jumla ya matoleo ya watu wengine yalikuwa ni darkoni 20,000 za dhahabu, mane 2,000 za fedha, na mavazi sitini na saba ya makuhani. BIBLIA KISWAHILI Na mabaki ya watu wakatoa darkoni za dhahabu elfu ishirini, na mane za fedha elfu mbili, na mavazi ya makuhani sitini na saba. |
Basi Hilkia kuhani, na Ahikamu, na Akbori, na Shafani, na Asaya, wakamwendea Hulda, nabii wa kike, mkewe Shalumu, mwana wa Tikva, mwana wa Harhasi, mtunza mavazi ya mfalme; (naye alikaa Yerusalemu katika mtaa wa pili;) wakasema naye.
Hata ulipowadia mwezi wa saba, na wana wa Israeli walipokuwa katika miji yao, watu wakakusanyika pamoja huko Yerusalemu.
Na watu waliosalia, makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, Wanethini, na hao wote waliojitenga katika watu wa nchi kwa Torati ya Mungu; wake zao, na wana wao, na binti zao, kila mwenye maarifa na akili;
Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa wakatoa, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu elfu ishirini, na mane za fedha elfu mbili na mia mbili.
Hivyo makuhani, na Walawi, na mabawabu, na waimbaji, na baadhi ya watu, na Wanethini, na Israeli wote, wakakaa mijini mwao. Hata ulipowadia mwezi wa saba, wana wa Israeli walikuwa wakikaa katika miji yao.