Hivyo Israeli wote walihesabiwa kwa nasaba; na tazama, hizo zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli; na Yuda wakachukuliwa mateka mpaka Babeli, kwa sababu ya makosa yao.
Nehemia 7:64 - Swahili Revised Union Version Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hao walitafuta orodha yao kati ya wengine walioorodheshwa katika kumbukumbu za koo, lakini ukoo wao haukuwemo. Kwa hiyo hawakuruhusiwa kutiwa katika huduma ya ukuhani kwani walihesabiwa kuwa najisi. Biblia Habari Njema - BHND Hao walitafuta orodha yao kati ya wengine walioorodheshwa katika kumbukumbu za koo, lakini ukoo wao haukuwemo. Kwa hiyo hawakuruhusiwa kutiwa katika huduma ya ukuhani kwani walihesabiwa kuwa najisi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hao walitafuta orodha yao kati ya wengine walioorodheshwa katika kumbukumbu za koo, lakini ukoo wao haukuwemo. Kwa hiyo hawakuruhusiwa kutiwa katika huduma ya ukuhani kwani walihesabiwa kuwa najisi. Neno: Bibilia Takatifu Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa ukuhani, kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. Neno: Maandiko Matakatifu Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani, kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. BIBLIA KISWAHILI Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi. |
Hivyo Israeli wote walihesabiwa kwa nasaba; na tazama, hizo zimeandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli; na Yuda wakachukuliwa mateka mpaka Babeli, kwa sababu ya makosa yao.
Uwakumbuke, Ee Mungu wangu, jinsi walivyounajisi ukuhani, na agano la ukuhani na la Walawi.
Mungu wangu akanitia moyoni mwangu, kwamba niwakusanye wakuu na maofisa, na watu, ili wahesabiwe kwa nasaba. Nikakiona kitabu cha vizazi vya hao waliokwea hapo kwanza, nikaona ya kwamba imeandikwa humo;
Tena katika makuhani; Wana wa Habaya, wana wa Hakosi, wana wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo wa binti za Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao.
Na huyo Tirshatha akawaambia kwamba wasile katika vile vitu vitakatifu sana, hata atakaposimama kuhani mwenye Urimu na Thumimu.
kama kuhani aliyetiwa mafuta akifanya dhambi, hata analeta hatia juu ya watu; ndipo na atoe kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya, na kumsongeza kwa BWANA ng'ombe dume mchanga mkamilifu, kuwa ni sadaka ya dhambi.