Ikawa, Daudi alipofika Mahanaimu, Shobi, mwana wa Nahashi wa Raba, wa wana wa Amoni, na Makiri, mwana wa Amieli wa Lo-debari, na Barzilai, Mgileadi wa Rogelimu,
Nehemia 7:63 - Swahili Revised Union Version Tena katika makuhani; Wana wa Habaya, wana wa Hakosi, wana wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo wa binti za Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wazawa wa koo zifuatazo za makuhani pia walirudi: Ukoo wa Hobaya, wa Hakozi na wa Barzilai (aliyekuwa ameoa binti za Barzilai, Mgileadi, naye akachukua jina la ukoo huo). Biblia Habari Njema - BHND Wazawa wa koo zifuatazo za makuhani pia walirudi: Ukoo wa Hobaya, wa Hakozi na wa Barzilai (aliyekuwa ameoa binti za Barzilai, Mgileadi, naye akachukua jina la ukoo huo). Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wazawa wa koo zifuatazo za makuhani pia walirudi: ukoo wa Hobaya, wa Hakozi na wa Barzilai (aliyekuwa ameoa binti za Barzilai, Mgileadi, naye akachukua jina la ukoo huo). Neno: Bibilia Takatifu Kutoka miongoni mwa makuhani: wazao wa Hobaya, wa Hakosi na wa Barzilai (mtu aliyemwoa binti Barzilai Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo). Neno: Maandiko Matakatifu Na kutoka miongoni mwa makuhani: wazao wa Hobaya, Hakosi na Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo). BIBLIA KISWAHILI Tena katika makuhani; Wana wa Habaya, wana wa Hakosi, wana wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo wa binti za Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao. |
Ikawa, Daudi alipofika Mahanaimu, Shobi, mwana wa Nahashi wa Raba, wa wana wa Amoni, na Makiri, mwana wa Amieli wa Lo-debari, na Barzilai, Mgileadi wa Rogelimu,
Lakini uwafanyie mema wana wa Barzilai Mgileadi, wawe miongoni mwao walao mezani pako; kwa jinsi walivyonijilia nilipokuwa nimekimbia mbele ya Absalomu, ndugu yako.
Na baada yao akaijenga Meremothi, mwana wa Uria, mwana wa Hakosi. Na baada yao akafanyiza Meshulamu, mwana wa Berekia, mwana wa Meshezabeli. Na baada yao akafanyiza Sadoki, mwana wa Baana.
Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi.