Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

1 Wafalme 2:7 - Swahili Revised Union Version

7 Lakini uwafanyie mema wana wa Barzilai Mgileadi, wawe miongoni mwao walao mezani pako; kwa jinsi walivyonijilia nilipokuwa nimekimbia mbele ya Absalomu, ndugu yako.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 “Lakini uwatendee mema wana wa Barzilai, Mgileadi, na uwatunze kwa ukarimu wawe kati ya wale wanaokula mezani pako; kwa sababu walinitendea mema wakati nilipomkimbia ndugu yako Absalomu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 “Lakini uwatendee mema wana wa Barzilai, Mgileadi, na uwatunze kwa ukarimu wawe kati ya wale wanaokula mezani pako; kwa sababu walinitendea mema wakati nilipomkimbia ndugu yako Absalomu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 “Lakini uwatendee mema wana wa Barzilai, Mgileadi, na uwatunze kwa ukarimu wawe kati ya wale wanaokula mezani pako; kwa sababu walinitendea mema wakati nilipomkimbia ndugu yako Absalomu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 “Lakini uwaoneshe wema wana wa Barzilai wa Gileadi na uwaruhusu wawe miongoni mwa wale walao mezani pako. Walisimama nami nilipomkimbia ndugu yako Absalomu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 “Lakini uwaonyeshe wema wana wa Barzilai wa Gileadi na uwaruhusu wawe miongoni mwa wale walao mezani pako. Walisimama nami nilipomkimbia ndugu yako Absalomu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Lakini uwafanyie mema wana wa Barzilai Mgileadi, wawe miongoni mwao walao mezani pako; kwa jinsi walivyonijilia nilipokuwa nimekimbia mbele ya Absalomu, ndugu yako.

Tazama sura Nakili

1 Wafalme 2:7
15 Marejeleo ya Msalaba  

Ila unikumbuke mimi, utakapopata mema, ukanifanyie fadhili, nakuomba, ukanitaje kwa Farao, na kunitoa katika nyumba hii.

Kwa kuwa jamaa yote ya baba yangu walikuwa kama watu wa kufa tu mbele ya bwana wangu mfalme; ila uliniweka mimi mtumishi wako kati ya hao walao mezani pako. Basi ni haki gani sasa niliyo nayo, hata nimlilie mfalme zaidi?

Nawe utamlimia nchi hiyo, wewe, na wanao, na watumishi wako; nawe utamletea mjukuu wa bwana wako matunda yake, apate chakula ale; lakini Mefiboshethi, mjukuu wa bwana wako, atakula chakula mezani pangu siku zote. Basi huyo Siba alikuwa na wana kumi na watano na watumishi ishirini.

Daudi akamwambia, Usiogope, maana bila shaka nitakutendea mema; kwa ajili ya Yonathani, baba yako, nami nitakurudishia mashamba yote ya Sauli, babu yako; nawe utakula chakula mezani pangu daima.

naye akambadilishia mavazi yake ya gerezani, akala chakula mbele yake daima, siku zote za maisha yake.

Na kwa posho yake, alipewa posho ya daima na mfalme, siku kwa siku sehemu, siku zote za maisha yake.

Tena wa makuhani; wazawa wa Habaya, wazawa wa Hakosi, wazawa wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo wa binti Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao.

Usimwache rafiki yako mwenyewe, wala rafiki ya baba yako, Wala usiende nyumbani mwa ndugu yako siku ya msiba wako. Afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali.

Naye akabadili mavazi yake ya gerezani, akala chakula mbele yake daima, siku zote za maisha yake.

Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo