Ikawa malango ya Yerusalemu yalipoanza kuwa na giza kabla ya sabato, niliamuru milango ifungwe, nikaamuru isifunguliwe hata sabato iishe; na baadhi ya watumishi wangu nikawaweka juu ya malango, ili usiingizwe mzigo wowote siku ya sabato.
Nehemia 7:3 - Swahili Revised Union Version Nikawaambia, Yasifunguliwe malango ya Yerusalemu kabla jua halijachomoza; na kabla walinzi hawajaondoka waifunge milango, mkaikaze; kisha wekeni walinzi wa zamu wa hao wakaao Yerusalemu, kila mtu na zamu yake, na kila mtu kuielekea nyumba yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema nikawaagiza, “Malango yasifunguliwe usiku kucha hadi jua linapokuwa limepanda. Kabla hawajaondoka walinzi ni lazima kufunga milango yote kwa makomeo yake. Teueni walinzi miongoni mwa wakazi wa mji wa Yerusalemu, kila mmoja awe mahali pake kukabiliana na nyumba yake.” Biblia Habari Njema - BHND nikawaagiza, “Malango yasifunguliwe usiku kucha hadi jua linapokuwa limepanda. Kabla hawajaondoka walinzi ni lazima kufunga milango yote kwa makomeo yake. Teueni walinzi miongoni mwa wakazi wa mji wa Yerusalemu, kila mmoja awe mahali pake kukabiliana na nyumba yake.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza nikawaagiza, “Malango yasifunguliwe usiku kucha hadi jua linapokuwa limepanda. Kabla hawajaondoka walinzi ni lazima kufunga milango yote kwa makomeo yake. Teueni walinzi miongoni mwa wakazi wa mji wa Yerusalemu, kila mmoja awe mahali pake kukabiliana na nyumba yake.” Neno: Bibilia Takatifu Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe hadi jua litakapokuwa limepanda. Walinzi wa malango wakiwa bado kwenye zamu, waamuru wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake, na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.” Neno: Maandiko Matakatifu Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe mpaka jua litakapokuwa limepanda. Walinzi wa malango wakiwa bado kwenye zamu, waamuru wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake, na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.” BIBLIA KISWAHILI Nikawaambia, Yasifunguliwe malango ya Yerusalemu kabla jua halijachomoza; na kabla walinzi hawajaondoka waifunge milango, mkaikaze; kisha wekeni walinzi wa zamu wa hao wakaao Yerusalemu, kila mtu na zamu yake, na kila mtu kuielekea nyumba yake. |
Ikawa malango ya Yerusalemu yalipoanza kuwa na giza kabla ya sabato, niliamuru milango ifungwe, nikaamuru isifunguliwe hata sabato iishe; na baadhi ya watumishi wangu nikawaweka juu ya malango, ili usiingizwe mzigo wowote siku ya sabato.
Baada yao wakajenga Benyamini na Hashubu, kuielekea nyumba yao. Baada yao akajenga Azaria, mwana wa Maaseya, mwana wa Anania, kando ya nyumba yake.
ndipo nilimteua ndugu yangu Hanani, kuwa mwangalizi wa Yerusalemu akisaidiana na Hanania, jemadari wa ngome, kwa maana alikuwa mtu mwaminifu na mwenye kumcha Mungu kuliko wengi.
Basi mji ulikuwa wa nafasi nyingi, tena mkubwa; lakini watu waliomo walikuwa wachache, na nyumba zilikuwa hazijajengwa.
BWANA asipoijenga nyumba Waijengao wanafanya kazi bure. BWANA asipoulinda mji Yeye aulindaye anakesha bure.
Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwamwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.