Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.
Nehemia 4:9 - Swahili Revised Union Version Bali sisi tulimwomba dua Mungu wetu, tena tukaweka walinzi, mchana na usiku, kwa sababu yao, ili kuwapinga. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ndipo tulipomwomba Mungu wetu na kuweka ulinzi dhidi yao, mchana na usiku. Biblia Habari Njema - BHND Ndipo tulipomwomba Mungu wetu na kuweka ulinzi dhidi yao, mchana na usiku. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ndipo tulipomwomba Mungu wetu na kuweka ulinzi dhidi yao, mchana na usiku. Neno: Bibilia Takatifu Lakini tulimwomba Mungu wetu, na tukaweka ulinzi usiku na mchana kupambana na tishio hili. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini tulimwomba Mungu wetu, na tukaweka ulinzi usiku na mchana kupambana na tishio hili. BIBLIA KISWAHILI Bali sisi tulimwomba dua Mungu wetu, tena tukaweka walinzi, mchana na usiku, kwa sababu yao, ili kuwapinga. |
Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.
Lakini Yuda wakasema, Nguvu zao wapagazi zimedhoofika, bado kuna vifusi tele; hatuwezi kuujenga ukuta.
Nao adui zetu wakasema, Hawatajua wala kuona, hadi tutakapokuja kati yao, na kuwaua, na kuikomesha kazi hiyo.
Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.
Muwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka zunguka, akitafuta mtu ammeze.