Waimbaji wakakusanyika kutoka uwanda na viunga vya Yerusalemu, na kutoka vijiji vya Wanetofathi;
Nehemia 3:22 - Swahili Revised Union Version Na baada yake wakafanyiza makuhani, watu wa Uwandani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sehemu inayofuata ilijengwa upya na makuhani waliokaa katika sehemu tambarare. Biblia Habari Njema - BHND Sehemu inayofuata ilijengwa upya na makuhani waliokaa katika sehemu tambarare. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sehemu inayofuata ilijengwa upya na makuhani waliokaa katika sehemu tambarare. Neno: Bibilia Takatifu Baada yake, ukarabati ulifanywa na makuhani waliotoka eneo lililouzunguka mji. Neno: Maandiko Matakatifu Baada yake, ukarabati ulifanywa na makuhani waliotoka eneo lililouzunguka mji. BIBLIA KISWAHILI Na baada yake wakafanyiza makuhani, watu wa Uwandani. |
Waimbaji wakakusanyika kutoka uwanda na viunga vya Yerusalemu, na kutoka vijiji vya Wanetofathi;
Baada yake akajenga Meremothi, mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, sehemu nyingine, kutoka mlangoni mwa nyumba ya Eliashibu mpaka mwisho wa nyumba ya Eliashibu.
Baada yao wakajenga Benyamini na Hashubu, kuielekea nyumba yao. Baada yao akajenga Azaria, mwana wa Maaseya, mwana wa Anania, kando ya nyumba yake.
Sanbalati na Geshemu wakatuma wajumbe kwangu, wakasema, Njoo, tukutane huko vijijini katika nchi tambarare ya Ono. Lakini wakakusudia kunifanyia mabaya.