Basi mambo yote ya Hezekia yaliyosalia, na ushujaa wake wote, tena alivyolifanya birika na mfereji, akaleta maji ndani ya mji, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Yuda?
Nehemia 3:16 - Swahili Revised Union Version Baada yake akajenga Nehemia, mwana wa Azbuki, mkuu wa nusu ya mtaa wa Beth-suri, mpaka mahali paelekeapo makaburi ya Daudi, na mpaka birika lililofanyizwa, na mpaka nyumba ya wapiganaji. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sehemu inayofuata hadi kwenye makaburi ya Daudi, bwawa na majengo ya jeshi ilijengwa upya na Nehemia, mwana wa Azbuki, mkuu wa nusu ya wilaya ya Beth-suri. Biblia Habari Njema - BHND Sehemu inayofuata hadi kwenye makaburi ya Daudi, bwawa na majengo ya jeshi ilijengwa upya na Nehemia, mwana wa Azbuki, mkuu wa nusu ya wilaya ya Beth-suri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sehemu inayofuata hadi kwenye makaburi ya Daudi, bwawa na majengo ya jeshi ilijengwa upya na Nehemia, mwana wa Azbuki, mkuu wa nusu ya wilaya ya Beth-suri. Neno: Bibilia Takatifu Baada yake, Nehemia mwana wa Azbuki, mtawala wa nusu ya wilaya ya Beth-Suri, alikarabati kufikia mkabala na makaburi ya Daudi, hadi kwenye bwawa lililotengenezwa, na kufikia Nyumba ya Mashujaa. Neno: Maandiko Matakatifu Baada yake, Nehemia mwana wa Azbuki, mtawala wa nusu ya wilaya ya Beth-Suri, alikarabati kufikia mkabala na makaburi ya Daudi, mpaka kwenye bwawa lililotengenezwa, na kufikia Nyumba ya Mashujaa. BIBLIA KISWAHILI Baada yake akajenga Nehemia, mwana wa Azbuki, mkuu wa nusu ya mtaa wa Beth-suri, mpaka mahali paelekeapo makaburi ya Daudi, na mpaka birika lililofanyizwa, na mpaka nyumba ya wapiganaji. |
Basi mambo yote ya Hezekia yaliyosalia, na ushujaa wake wote, tena alivyolifanya birika na mfereji, akaleta maji ndani ya mji, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Yuda?
Wakamzika katika makaburi yake mwenyewe, aliyojichimbia katika mji wa Daudi, wakamlaza juu ya kitanda kilichojazwa manukato, na kila namna ya machanganyiko ya hao mafundi wa dawa; wakawasha moto mkubwa sana kwa heshima yake.
Kisha nikaendelea mpaka lango la chemchemi, na ziwa la mfalme; lakini hapakuwa na nafasi ya kupita kwa yule mnyama niliyemganda.
Na baada yake akajenga Shalumu, mwana wa Haloheshi, mtawala wa nusu ya sehemu ya Yerusalemu, yeye na binti zake.
Na lango la jaa akalijenga Malkiya, mwana wa Rekabu, mtawala wa sehemu ya wa Beth-hakeremu; akalijenga, akaisimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake.
Baada yake wakajenga Walawi, Rehumu, mwana wa Bani. Baada yake akajenga Hashabia, mkuu wa nusu ya mtaa wa Keila, kwa mtaa wake.
Nanyi mlifanya birika la maji katikati ya kuta mbili, la kuwekea maji ya birika la kale; lakini hamkumwangalia yeye aliyeyafanya hayo, wala kumjali yeye aliyeyatengeneza zamani.
Nanyi mlipaona mahali palipobomoka katika mji wa Daudi ya kuwa ni pengi, nanyi mliyakusanya maji ya birika la chini.
Basi BWANA akamwambia Isaya, Haya, toka, umlaki Ahazi, wewe na Shear-yashubu mwana wako, huko mwisho wa mfereji wa birika la juu, katika njia kuu ya Uwanja wa Dobi;
Wanaume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo.