Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Nehemia 2:14 - Swahili Revised Union Version

14 Kisha nikaendelea mpaka lango la chemchemi, na ziwa la mfalme; lakini hapakuwa na nafasi ya kupita kwa yule mnyama niliyemganda.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Halafu, nikaenda kwenye Lango la Chemchemi na kwenye Bwawa la Mfalme. Lakini yule punda niliyempanda hakuweza kupita.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Halafu, nikaenda kwenye Lango la Chemchemi na kwenye Bwawa la Mfalme. Lakini yule punda niliyempanda hakuweza kupita.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Halafu, nikaenda kwenye Lango la Chemchemi na kwenye Bwawa la Mfalme. Lakini yule punda niliyempanda hakuweza kupita.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Kisha nikaelekea hadi Lango la Chemchemi na Bwawa la Mfalme, lakini hapakuwa na nafasi ya kutosha mnyama wangu kupita,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kisha nikaelekea mpaka Lango la Chemchemi na Bwawa la Mfalme, lakini hapakuwepo nafasi ya kutosha kwa ajili ya mnyama wangu kupita,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Kisha nikaendelea mpaka lango la chemchemi, na ziwa la mfalme; lakini hapakuwa na nafasi ya kupita kwa yule mnyama niliyempanda.

Tazama sura Nakili




Nehemia 2:14
7 Marejeleo ya Msalaba  

Mfalme wa Ashuru akawatuma jemadari wake, na mkuu wa matowashi, na kamanda wake, toka Lakishi, kwa mfalme Hezekia huko Yerusalemu, pamoja na jeshi kubwa. Nao wakakwea wakafika Yerusalemu. Na walipokwisha kufika, wakaja wakasimama karibu na mfereji wa birika la juu, lililo katika njia kuu ya kuuendea Uwanda wa Dobi.


Basi mambo yote ya Hezekia yaliyosalia, na ushujaa wake wote, tena alivyolifanya birika na mfereji, akaleta maji ndani ya mji, je! Hayakuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Yuda?


Naye huyo Hezekia ndiye aliyezuia chemchemi ya juu ya maji ya Gihoni, akayaleta chini moja kwa moja upande wa magharibi wa mji wa Daudi. Akafanikiwa Hezekia katika kazi zake zote.


na kwa lango la chemchemi, wakienda moja kwa moja mbele yao, wakapanda madaraja ya mji wa Daudi, uinukapo ukuta, juu ya nyumba ya Daudi, mpaka lango la maji upande wa mashariki.


Na lango la chemchemi akalijenga Shalumu, mwana wa Kolhoze, mkuu wa Mispa akalitengeneza lango la Chemchemi akalijenga na kulifunika, akasimamisha milango yake, na vyuma vyake, na makomeo yake, na huo ukuu wa birika la Shiloa karibu na bustani ya mfalme, mpaka madaraja yashukayo kutoka mji wa Daudi.


Baada yake akajenga Nehemia, mwana wa Azbuki, mkuu wa nusu ya mtaa wa Beth-suri, mpaka mahali paelekeapo makaburi ya Daudi, na mpaka birika lililofanyizwa, na mpaka nyumba ya wapiganaji.


nikajifanyia mabwawa ya maji, ya kuunyweshea msitu mlimopandwa miti michanga.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo