Tena hawa ndio waimbaji, wakuu wa koo za baba zao katika Walawi, ambao walikaa vyumbani, kisha walikuwa hawana kazi nyingine; kwa kuwa walifanya kazi yao mchana na usiku.
Nehemia 12:8 - Swahili Revised Union Version Tena Walawi; Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda, na Matania, aliyekuwa juu ya shukrani, yeye na ndugu zake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walawi: Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda na Matania, ambaye alihusika na usimamizi wa nyimbo za shukrani akishirikiana na ndugu zake. Biblia Habari Njema - BHND Walawi: Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda na Matania, ambaye alihusika na usimamizi wa nyimbo za shukrani akishirikiana na ndugu zake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walawi: Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda na Matania, ambaye alihusika na usimamizi wa nyimbo za shukrani akishirikiana na ndugu zake. Neno: Bibilia Takatifu Walawi walikuwa Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda, na pia Matania, ambaye pamoja na wenzake, alikuwa kiongozi wa nyimbo za shukrani. Neno: Maandiko Matakatifu Walawi walikuwa Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda, na pia Matania, ambaye pamoja na wenzake, alikuwa kiongozi wa nyimbo za shukrani. BIBLIA KISWAHILI Tena Walawi; Yeshua, Binui, Kadmieli, Sherebia, Yuda, na Matania, aliyekuwa juu ya shukrani, yeye na ndugu zake. |
Tena hawa ndio waimbaji, wakuu wa koo za baba zao katika Walawi, ambao walikaa vyumbani, kisha walikuwa hawana kazi nyingine; kwa kuwa walifanya kazi yao mchana na usiku.
Ndipo akasimama Yoshua, mwana wa Yosadaki, na ndugu zake makuhani, na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na ndugu zake, nao wakaijenga madhabahu ya Mungu wa Israeli, ili kutoa sadaka za kuteketezwa juu yake, kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, mtu wa Mungu.
na Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zikri, mwana wa Asafu, mkuu wa kuanzisha shukrani katika sala, na Bakbukia, wa pili wake miongoni mwa nduguze; na Obadia, mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni.
Naye msimamizi wa Walawi huko Yerusalemu, ni Uzi, mwana wa Bani, mwana wa Hashabia, mwana wa Matania, mwana wa Mika, wa wana wa Asafu, hao waimbaji, alikuwa juu ya kazi ya nyumba ya Mungu.
Nao wakuu wa Walawi; Hashabia, Sherebia, Yeshua, Binui, Kadmieli, na ndugu zao kuwaelekea, ili kusifu na kushukuru, kama amri ya Daudi, mtu wa Mungu, zamu kwa zamu.
Salu, Amoki, Hilkia, Yedaya. Hawa walikuwa wakuu wa makuhani na ndugu zao siku za Yoshua.
Ndipo wakasimama katika jukwaa la Walawi, Yeshua, na Bani, na Kadmieli, na Shebania, na Buni, na Sherebia, na Bani, na Kenani, wakamlilia BWANA, Mungu wao, kwa sauti kuu.